Shirika la ndege la China Southern laanza safari kwenda Nairobi
Wizara ya Afya ya Kenya imesema, Shirika la Ndege la China Southern jana lilianza tena safari zake kwenda mjini Nairobi, Kenya, baada ya kusitishwa kwa wiki mbili kutokana na mlipuko wa virusi vya korona.
Abiria wote 239 waliopanda ndege hiyo walikaguliwa, kupimwa joto, na kuruhusiwa huku wakipewa ushauri wa kukaa nyumbani kwa siku 14 zijazo kufuatilia afya zao.
Walipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, abiria hao walifanyiwa uchunguzi kabla ya kuruhusiwa kutoka nje ya uwanja huo
Wakati huohuo, ndege ya mizigo ya Shirika la Ndege la Ethiopia iliyobeba tani 50 za vifaa vya matibabu iliwasili mjini Guangzhou, China siku ya ijumaa, ikiwa ni ndege ya 24 ya mizigo kuja China baada ya mlipuko wa virusi vya korona kutokea.
Tangu Januari 24 hadi sasa, Shirika hilo la ndege limeendelea na safari zake za moja kwa moja na kusafirisha karibu tani 1,400 za vifaa vya kuzuia na kudhibiti kuenea kwa mlipuko wa virusi vya korona nchini China.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |