Kwanini Guinea-Bissau ina marais wawili?
Kura zilikusudiwa kufuta kumbukumbu ya yaliyopita, lakini badala yake, zimesababisha mgogoro mpya wa kisiasa katika taifa ambalo Jeshi limekuwa na ushawishi wa kisiasa.
Tume ya uchaguzi nchini humo ilimtangaza bwana Embalo kuwa amemshinda mpinzani wake, Domingos Simoes Pereira kwa asilimia 54% kwa 46% katika uchaguzi wa duru ya pili mwezi Disemba tarehe 29.
Wafuasi wa bwana Embaló wakishangilia baada ya kutangazwa mshindi
Rais aliyeondoka madarakani José Mário Vaz alikabidhi madaraka kwa Bwana Embaló katika sherehe zilizofanyika katika hoteli ya kifahari siku ya Alhamisi.
Lakini Bwana Pereira wa chama cha PAIGC, kilichoiongoza Guinea-Bissau kupata uhuru wake na kilichokuwa pekee mpaka 1990, alikataa kuapishwa kwa Embaló, akisema uchaguzi ulitawaliwa na udanganyifu.
Kisha kikatumia wingi wa idadi ya wabunge kumuapisha bwana Cassamá, spika wa bunge kuwa rais wa mpito, mpaka Mahakama ya juu ilipotoa uamuzi kuhusu ombi la kubatilisha ushindi wa Embaló.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |