Wasimamizi wa sekta ya fedha wazindua daftari la kudumu la watoa huduma za kifedha (FSR)
Wasimamizi wa sekta ya fedha Tanzania wakiungwa mkono na Mfuko wa kuendeleza sekta ya Fedha Tanzania, wamezindua Daftari la kudumu la watoa huduma za kifedha , ambalo lengo ni kuonyesha mahali ambapo vituo vinavyotoa huduma za kifedha vinapatikana kwenye nchi.
FSR ni daftari endelevu ambalo litaonyesha mahali ambapo vituo vinavyotoa huduma za kifedha vinapatikana kwa nchi nzima kwa kukamata tarakimu za kijiografia zinazoonyesha eneo na aina ya huduma inayopatikana ambalo lengo lake ni kufungulia uwezo wa takwimu za kijiografia kama kifaa kwa ajili ya intelijensia ya kibiashara, kufanya maamuzi na mipango mikakati.
Wasimamizi wakiongozwa na Benki kuu ya Tanzania inajumuisha Tume ya maendelo ya ushirika (TCDC), Mamlaka ya usimamizi wa bima Tanzania (TIRA) na Mamlaka ya masoko ya mitaji na dhamana (CMSA).
Benki kuu ya Tanzania pamoja na mwenyekiti wa Tume ya taifa ya huduma jumuishi za kifedha, Profesa Florens Luoga, alizindua mfumo wa daftari la kudumu la watoa huduma za kifedha kwa kukuza kauli mbiu ya "Takwimu ni Mafuta mapya" na ambao wataitumia ipasavyo na kwa manufaa yao watavuna matunda yake na kukua"
Alisema kuwa daftari la kudumu la watoa huduma za kifedha italeta machine ambayo itakusanya na kufungulia nguvu ya takwimu ili kuhimiza ukuaji, ubunifu na ushirikiano ndani ya sekta ya fedha Tanzania ambayo iko tayari kwa ajili ya muongo huu wa kidijitali, viwanda na muunganisho
FSR itakuwa daftari la kwanza la aina yake katika nchi za afrika chini ya jangwa la sahara ambalo litaendesha lenyewe mchakato wa kukusanya takwimu na kutoa upatikanaji wa taarifa kwa kidijitali moja kwa moja. Ingawa daftari litatumika kama mfumo wa taifa wa kufuatilia ukuaji na mgawanyo wa vituo vinavyotoa huduma za kifedha na kuwataarifu wadau wakuu wa Mpango wa taifa wa huduma jumuishi za kifedha kwa mwaka 2018-2022 na umma kwa ujumla.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |