• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Machi 21-Machi 27)

    (GMT+08:00) 2020-03-27 20:11:42

    Jack Ma aahidi kusaidia vita dhidi ya Corona Afrika

    Bilionea wa China Bw. Jack Ma ambaye ni mwanzilishi mwenza wa kampuni ya Alibaba ya China wiki hii aliahidi kutoa vifaa vya upimaji zaidi ya milioni moja kwa bara la Afrika. Ahadi hiyo inakuja wakati ambapo nchi za Afika zinafunga mipaka kutokana na hofu ya athari ya maambukizi ya virusi vya Corona,

    Mpaka sasa bara hilo lenye idadi ya watu bilioni 1.3 limeripoti maambukizi karibu 1,100 katika nchi 43, na watu 39 kati yao wamefariki. Idadi hiyo ni sehemu ndogo katika idadi ya maambukizi ya watu 305,000 kote duniani. Taarifa iliyotolewa na mfuko wa Jack Ma inasema, kampuni hiyo haiwezi kupuuza hatari inayowezekana kutokea barani Afrika, na kufikiri bara hilo litaepuka ugonjwa huo, na dunia haiwezi kumudu matokeo mabaya ya maambukizi ya Corona barani Afrika. Rais Paul Kagame wa Rwanda kwenye ukurusa wake wa Twitter ameushukuru mfuko wa Jack Ma kwa kutoa vifaa vya upimaji wa virusi vya Conona. Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed wiki iliyopita aliahidi kusambaza vifaa hivyo kwa nchi nyingine za Afrika.


    1  2  3  4  5  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako