Kenya yasema kilele cha ugonjwa wa COVID-19 ni katika miezi ya Agosti na Septemba
Kenya imewatahadharisha raia wake kuwa kilele cha ugonjwa wa Covid 19 kitakuwa miezi ya Agosti hadi Septemba ambapo watakuwa wakirekodi waathirika karibia 200 kwa siku. Mkurugenzi wa Afya ya Umma Patrick Amoth, amesema maambukizi yameingia katika ngazi ya kijamii ambayo ni hatari zaidi.
Janga la corona bado linajidhihirisha kuwa changamoto katika mataifa mengi duniani. Kenya nayo haijaachwa. Katika siku za hivi karibuni, Kenya imekuwa ikirekodi waathiriwa wengi zaidi waliopata maambukizi ikilinganishwa na awali.
Hivi sasa Kenya inapanga kuanza kupima watu zaidi ya 3,000 kwa siku kuanzia hivi karibuni. Hilo linajitokeza wakati ambapo wizara ya afya imedokeza kuwa na vifaa vya kutosha vya kupima virusi vya corona ambavyo vinaweza kudumu hata kwa mwezi mzima.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |