Serikali ya Marekani kujitoa kwenye Mkataba wa Anga huru.
Serikali ya Marekani imetangaza kujiondoa kwenye mkataba wa Anga Huru duniani. Kwa mujibu wa kanuni za kujitoa kwenye mkataba huo, Marekani itajitoa rasmi kwenye mkataba huo baada ya miezi sita.
Mkataba huo ulioanza kutekelezwa mwaka 2002, unaruhusu ndege za uchunguzi zisizo na silaha za nchi zilizosaini mkataba huo kuruka kwenye anga ya nchi nyingine mwanachama kama hatua za kujenga uaminifu.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Russia Bi. Maria Zakharova, amesema Russia inasubiri Marekani kufafanua kujitoa kwenye Mkataba wa Anga huru.
Bi. Zakharova amesema Russia bado haijapokea taarifa rasmi au ufafanuzi kutoka Marekani. Mkataba huo wa kimataifa una muundo wa utekelezaji, na umeweka majukumu yaliyothibitishwa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |