Rais Donald Trump ashtakiwa
Makundi ya kutetea haki za binadamu nchini Marekani yamewasilisha kesi dhidi ya Rais Donald Trump kwa kumshtaki baada ya vikosi vya usalama kuwarushia mabomu ya moshi waandamanaji waliokuwa wakiandamana kwa amani nje ya Ikulu ya White House.
Umoja wa Uhuru wa Raia wa Marekani, ACLU pamoja na makundi mengine, yalimshtumu rais huyo na maafisa wakuu serikalini kwa kukiuka haki za waandamanaji hao waliokuwa wakiendesha kampeni inayojulikana kama maisha ya watu weusi ni muhimu pamoja na waandamanaji wengine wa kibinafsi.
Mkurugenzi wa masuala ya kisheria katika umoja huo wa ACLU Scott Michelman amesema kuwa matamshi ya "kiuhalifu" ya Trump dhidi ya waandamanaji hao kwasababu anatofautiana na maoni yao yanatikisa msingi wa mpangilio wa kikatiba nchini humo.
Waandamanaji hao wamekuwa wakifanya maandamano nchini humo katika siku za hivi karibuni kuelezea kughadhabishwa kwao na kifo cha Mmarekani mweusi George Floyd mikononi mwa polisi katika jimbo la Minnesota.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |