• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Mei 30-Juni5 )

    (GMT+08:00) 2020-06-05 19:57:07

    Tanzania yasimamisha shughuli katika mpaka wa Namanga

    Mpaka wa Namanga upande wa Tanzania umesitisha shughuli zote za kibiashara na nchi jirani ya Kenya kwa muda kutokana na nchi hiyo kutoamini vyeti vya ugonjwa Corona vya madereva wa malori wa Tanzania vinavyoonyesha kuwa hawajaambukizwa.

    Mkuu wa Wilaya ya Longido ,Frank Mwaisumbe,amesema kuwa hatua hiyo imefikiwa baada ya upande wa Kenya kukiuka makubaliano ya pande hizo mbili,waliyotiliana saini Mei,mwaka huu,kwa kuzuia madereva wa Tanzania ,kukataa vyeti ili wawaruhusu kuingia Kenya.

    Katika makubaliano hayo,waliamua katika lori itaruhusiwa dereva na wasaidizi wawili kuingia katika nchi husika wote wakiwa wamepimwa kama wana maambukizo ya Corona.

    Hata hivyo,Mwaisumbe alisema upande wa Kenya wamebadilika kwa kuwazuia na kutaka kuwapima tena.

    Alisema kama hali ya kutoaminiana itaendelea itwalazimu kutoa uamuzi wa kuigeuza Namanga kuwa bandari kavu na majirani wakenya watashusha mizigo au bidhaa upande wake na Tanzania kuichukua na pia hata Tanzania itaacha mizigo upande wake ili Kenya waifuate.


    1  2  3  4  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako