Mtandao wa kijamii wa Facebook umeondoa mtandaoni matangazo ya kampeni ya rais Donald Trump kwa kutumia alama zilizokuwa za utawala wa kinazi wa Ujerumani.
Facebook imesema tangazo lililolengwa lilikuwa na alama ya pembe tatu nyekundu kama iliyotumika na utawala wa kinazi kuwatambua wapinzani wao kama wakomunisti.
Matangazo hayo ni sehemu ya kampeni ya Trump kwa uchaguzi wa Novemba mwaka huu.
Timu ya kampeni ya Trump imesema kuwa tangazo hilo lilikuwa linakilenga kikundi cha wanaharakati wa mrengo wa kushoto antifa, ambacho wanadai kinatumia nembo hiyo.
Facebook inadai matangazo hayo yanaenda kinyume na sera yake ya chuki ya kupangwa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |