Rais mpya wa Burundi aapishwa rasmi
Hatimaye nchi ya Burundi imemuapisha rasmi rais mpya wa taifa hilo Evariste Ndayishimiye, katika hafla iliyohuguriwa umati mkubwa wa watu pamoja na baadhi ya viongozi kutoka mataifa tofauti.
Akizunguma baada ya kula kiapo hicho , rais Evariste amesema kwamba atapatia kipaumbele haki za kibinadamu.
Amesisitiza kuwa mataifa ya kigeni hayafai kumkumbusha kuhusu suala hilo kwa kuwa ndio suala atakalolipa kipaumbele.
Amevionya vyama vya upinzani dhidi ya kuzua ghasia nchini humo. Evariste Ndayishimiye vilevile aliviomba vyombo vya habari na wanaharakati wa haki za kibinadamu kushirikiana na serikali kukabiliana na matatizo yanayokumba taifa hilo, la sivyo vitaonekana kufanyiakazi watu wengine na sio raia wa Burundi. Bwana Ndayishimie aliongezea kwamba Burundi inapenda majirani wema.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |