Mahakama ya juu ya Burundi imemhukumu kifungo cha maisha rais wa zamani wa nchi hiyo, Meja Pierre
Mahakama ya juu ya Burundi imemhukumu kifungo cha maisha rais wa zamani wa nchi hiyo, Meja Pierre Buyoya baada ya kumkuta na hatia ya kumuuwa mrithi wake, Melchior Ndadaye mwaka 1993. Hata hivyo, Buyoya hakuwepo Burundi.
Mahakama hiyo imesema katika tangazo la hukumu hiyo dhidi ya Meja Pierre Buyoya, kuwa kiongozi huyo wa zamani amepewa kifungo cha maisha jela kutokana na mchango wake katika mapinduzi ya kijeshi ya mwaka 1993 dhidi ya Rais Melchior Ndadaye, ambaye alikuwa amekaa madarakani kwa miezi michache tu baada ya kumshinda Buyoya katika uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia kufanyika nchini Burundi, tangu nchi hiyo ilipopata uhuru wake kutoka ukoloni wa Kibelgiji mwaka 1962.
Hukumu hiyo iliyotangazwa kwenye mkesha wa kumbukumbu ya miaka 27 tangu kuuawa Ndadaye, imewahusisha pia maafisa wengine waandamizi wa zamani 18, wakiwemo wawili waliokuwa makamu wa rais, Bernard Busokoza na Alphonse Marie Kadege.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |