Rais wa Marekani Donald Trump amesema Sudan itaondolewa kwenye orodha ya mataifa yanayofadhili makundi ya kigaidi, ikiwa itakubali kutoa dola milioni 335 kuwalipa wahanga wa Kimarekani wa mashambulizi ya kigaidi.
Rais wa Marekani Donald Trump amesema Sudan itaondolewa kwenye orodha ya mataifa yanayofadhili makundi ya kigaidi, ikiwa itakubali kutoa dola milioni 335 kuwalipa wahanga wa Kimarekani wa mashambulizi ya kigaidi.
Hatua hiyo itafungua milango kwa nchi hiyo ya Afrika kupata mikopo ya kimataifa na misaada inayohitajika kufufua uchumi wake uliporomoka pamoja na kuisaidia nchi hiyo kuwa ya kidemokrasia.
Waziri Mkuu Abdalla Hamdok ameliunga mkono tangazo hilo la Trump.
Trump ametoa tamko hilo ikiwa zimebakia takriban wiki mbili hadi siku ya uchaguzi mkuu wa Marekani.
Marekani ilichukua uamuzi wa kuiweka Sudan katika orodha hiyo mnamo mwaka 1993, ikiamini rais wa wakati huo Omar al-Bashir alikuwa akifadhili makundi ya kigaidi.
Lakini wengi Sudan wanasema ni uamuzi uliopitwa na wakati, kwani Bashir aliondolewa madarakani mwaka jana, na taifa hilo limekuwa likitoa ushirikiano katika vita vya kupambana na ugaidi.
Kufuatia vuguvugu la maandamano ya mwaka jana yaliyomuondoa madarakani Bashir mnamo mwezi Aprili, Sudan hivi sasa inajaribu kuimarisha demokrasia lakini bado safari hiyo inayumba.
Serikali ya mpito ya kijeshi na raia hivi sasa ndiyo inayotawala nchi, huku kukiwa na matumainina ya kufanyika uchaguzi mwishoni mwa mwaka 2022.
Hamdok amesema walianza mazungumzo na Marekani mwaka jana, ambayo yalituama zaidi kwenye suala la pesa.
Na vyanzo vya kuaminika vimesema serikali ya Trump inaitaka Sudan iwalipe wahanga wa mashambulizi yaliyofanywa na mtandao wa al-Qaeda katika balozi za Marekani nchini Kenya na Tanzania mnamo mwaka 1998.
Kiongozi wa mtandao wa al-Qaida Osama bin Laden, inaaminika alikuwa akiiishi nchini Sudan wakati wa mashambulizi hayo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |