Rais Xi Jinping wa China na waziri mkuu wa Hungary Viktor Orbán wafanya mazungumzo mjini Budapest
2024-05-10 09:02:02| CRI

Rais Xi Jinping wa China na waziri mkuu wa Hungary Viktor Orbán jana Mei 9 walifanya mazungumzo mjini Budapest, ambapo wametangaza kuinua uhusiano kati ya nchi hizo mbili hadi kufikia ngazi ya Uhusiano wa Wenzi wa Kimkakati wa Pande Zote Kwa Hali Zote Katika Zama Mpya.

Rais Xi amebainisha kuwa, huu ni mwaka wa 75 tangu China na Hungary zianzishe uhusiano wa kibalozi, na umeleta fursa mpya na muhimu kwa maendeleo ya uhusiano kati yao. Nchi hizo mbili zinapaswa kuendelea kuwa marafiki wakubwa wa kuaminiana na wenzi wema wa kunufaishana, zinapaswa kutumia vyema fursa ya kuanzishwa kwa Uhusiano wa Wenzi wa Kimkakati wa Pande Zote Kwa Hali Zote Katika Zama Mpya, na kutia msukumo mpya na mkubwa kwenye ushirikiano kati ya nchi hizo mbili, ili kujenga siku njema za baadaye kwa ajili ya watu wa pande mbili.

Naye Waziri Orbán amesema, kupandishwa ngazi kwa uhusiano kati ya Hungary na China kutaweka mwelekeo kwa maendeleo ya uhusiano wa nchi hizo mbili, na ana imani kubwa na mustakbali wa uhusiano huo. Amesema, dhamira thabiti ya Hungary ya kuimarisha ushirikiano na China haiathiriwi na nguvu yoyote. Hungary inaipongeza China kwa mchango wake muhimu katika kuhimiza amani ya dunia, na inapenda kuongeza mawasiliano na uratibu na China, ili kulinda kwa pamoja amani na utulivu wa dunia.

Baada ya mazungumzo, viongozi hao wawali walishuhudia kubadilishana kwa nyaraka za ushirikiano zinazohusu “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, sekta za uchumi na biashara, uwekezaji, sayansi na teknolojia, utamaduni na kilimo.