Wakati mkutano wa kilele wa viongozi wa nchi za BRICS wa mwaka 2024 utakapofanyika, jukwaa la majopo ya washauri bingwa ya nchi za Kusini duniani lenye kaulimbiu ya “Amani, Maendeleo, Usalama, Kushikana Mikono Katika Kujenga Kwa Pamoja Dunia yenye Ustawi na Hatma ya Pamoja” lililoandaliwa na idara ya mawasiliano ya kimataifa ya kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Shirika kuu la Utangazaji la China CMG na televisheni ya CGTN limefanyika hapa Beijing. Mkuu wa idara ya mawasiliano ya kimataifa ya CPC Bw. Liu Jianchao na mkuu wa shirika la CMG Bw. Shen Haixiong wametoa hotuba kwa njia ya video. Viongozi, wajumbe wa serikali, wasomi wa majopo ya washauri bingwa na wajumbe wa vyombo vya habari kutoka nchi 76 duniani wamehudhuria au kushiriki kwenye kongamano hilo kwa njia ya mtandao.
Bw. Liu amesema, “Dunia ya Kusini inaendelea kukua, ikiwa ni matarajio ya nchi nyingi za Kusini, na ni mwelekeo wa maendeleo ya kihistoria na matumaini ya hali ya mabadiliko ya karne. China ikiwa moja ya nchi za kusini, siku zote ni mdhamini na mshiriki muhimu wa ushirikiano wa Kusini-Kusini. China itaendelea kuwa pamoja na nchi za Kusini na kutelekeza jukumu la “dunia ya Kusini”, kuhimiza utekelezaji wa Pendekezo la Maendeleo Duniani (GDI), Pendekezo la Usalama Duniani (GSI), na Pendekezo la Ustaarabu Duniani (GCI), ili kukusanya nguvu kubwa zaidi ya Dunia ya Kusini kwa ajili ya ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja.