Kamati ya Maendeleo na Mageuzi ya China yasema uchumi wa China unakua kwa utulivu
2024-10-08 15:03:45| cri

Mkurugenzi wa Kamati ya Maendeleo na Mageuzi ya China Bw. Zheng Shanjie amesema, katika mazingira ya sasa ya ndani na ya nje yenye utatanishi, uchumi wa China umeendelea kukua kwa utulivu, ambapo nguvu mpya ya uzalishaji inajengwa kwa haraka na maendeleo yenye ubora wa juu yanapiga hatua kwa kina.

Kwa mujibu wa ofisa huyo, kutokana na hali ya sasa, mwelekeo wa ukuaji wa uchumi wa China haujabadilika, na hali mbalimbali nzuri ikiwemo mustakabli mkubwa wa soko na ustahimilivu mkubwa wa kiuchumi pia hazijabadilika. Amesema, China ina imani kubwa ya kutimiza malengo ya kiuchumi ya mwaka, na pia ina imani kubwa ya kudumisha maendeleo endelevu ya uchumi.