Rais Xi asisitiza mafanikio zaidi ya kitaifa, mchango kwa amani na maendeleo ya binadamu
2024-10-01 09:03:51| CRI

Rais Xi Jinping wa China amesema Wachina watapata mafanikio makubwa zaidi na kutoa mchango mkubwa katika masuala matukufu ya amani na maendeleo ya binadamu.

Rais Xi ambaye pia katibu mkuu wa kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na mwenyekiti wa Kamisheni Kuu ya Kijeshi, ameyasema hayo kwenye hotuba aliyotoa kwenye jumba kuu la mikutano ya Umma mjini Beijing, wakati wa sherehe ya maadhimisho ya miaka 75 ya kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China (PRC).

Viongozi wengine waandamizi wa China ikiwa ni pamoja na waziri mkuu Li Qiang, Zhao Leji, Wang Huning, Cai Qi, Ding Xuexiang, Li Xi na Han Zheng, na wageni wapatao 3,000 wa China na kutoka nchi za nje walihudhuria sherehe hiyo.