Rais wa mpito wa Iran asema Iran inaazimia kuchangia uhuru na maendeleo ya Sudan
2024-05-27 08:40:02| CRI

Rais wa mpito wa Iran Mohammad Mokhber amesema nchi yake itafanya kila iwezavyo kuhakikisha inachangia uhuru, maendeleo na amani ya watu wa Sudan.

Hayo ameyasema siku ya Jumapili huko Tehran katika mkutano wake na Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan Hussein Awad Ali, akisisitiza majukumu muhimu ya hayati Rais Ebrahim Raisi wa Iran na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amir-Abdollahian katika kukuza uhusiano na ushirikiano wa nchi hiyo na Waislamu na madola yenye fikra sawa na hiyo, na kutilia mkazo kuwa njia hiyo hiyo itaendelea kufuatwa kama mkakati wa kimsingi wa Iran.

Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan, alitoa salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Raisi na ujumbe wake katika ajali ya helikopta Jumapili iliyopita, akisema uhusiano kati ya nchi yake na Iran umeanzishwa kwa kuzingatia kanuni za Kiislamu na kibinadamu pamoja na urafiki kati ya watu wa nchi hizo mbili.