Miili 7 imefukuliwa katika Msitu wa Shakahola nchini Kenya, ikiwa ni siku ya kwanza ya Awamu ya Tano ya Ufukuzi iliyoanza jana Jumatatu.
Mpasuaji Mkuu wa Serikali ya nchi hiyo Dkt Johansen Oduor amesema, makaburi 50 yametambuliwa na kwamba yatafukuliwa katika siku zijazo.
Watu hao wanaaminika kufa njaa baada ya kufunga bila kula wala kunywa kwa siku nyingi msituni kwa imani potofu kwamba watamuona Yesu, kulingana na mafundisho ya mhubiri tatanishi Paul Mackenzie, ambaye anashikiliwa na polisi kwa makosa ya mauaji na mafundisho ya itikadi kali.