Wanajeshi zaidi ya 100 wa Burkina Faso wauawa katika shambulizi la kundi mshirika wa al-Qaida
2024-06-17 09:08:05| CRI

Jumuiya ya intelijinsia iitwayo “Tafuta Makundi ya Kigaidi ya Kimataifa” (SITE) imesema kundi moja mshirika wa al-Qaida limedai kuhusika na shambulizi lililotokea Jumanne iliyopita na kusababisha vifo vya wanajeshi zaidi ya 100 wa Burkina Faso huko Mansila, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Taarifa iliyotolewa na jumuiya moja ya wanafunzi katika eneo hilo imesema, ‘watu wenye nia mbaya’ walishambulia eneo la kijeshi, nyumba na maduka.

Serikali ya Burkina Faso bado haijatoa taarifa kuhusu shambulizi hilo.