11: Mikoa ya Xinjiang na Tibet

Utamaduni wa Tibet

Tangka

Tangka ni tamshi la kitibet, nayo ni picha za rangi zilizotariziwa au kuchorwa kwenye vitambaa, hariri au karatasi. Picha hizo ni aina moja yenye mtindo wa utamaduni wa kabla la watibet.

Inasemekana kuwa, katika zama za kale, binti mfalme Wencheng alipoolewa Tibet, alikwenda na ufundi wa kufuma nguo, kutokana na picha hizo tunaweza kuona kuwa ufundi huo wa uzalishaji ulitumiwa na kuenea huko Tibet wakati huo. Rangi zilizotumika katika uchoraji wa picha hizo zilitengenezwa kwa njia ya kisayansi, ndani yake zilitiwa madini na mimea, tena hali ya hewa ya uwanda wa juu wa Tibet ni isiyo na unyevu, hivyo picha za Tangka hata zilichorwa karne kadhaa zilizopita, rangi zake bado zinaonekana ni nzuri za kupendeza kama zilivyo za picha mpya.

Yaliyochorwa kwenye Tangka yanahusu mambo yote ya maisha ya jamii, hata kama ni histoira ya jamii, na shughuli za kidini zimeoneshwa zaidi katika picha za Tangka.

Maua ya siagi

Maua ya siagi ni sanaa ya sanamu za mafuta. Sanaa hiyo inaonesha mambo mengi mbalimbali kuhusu hadithi za dini ya kibudha, hadithi ya Budha mkuu Sakyamuni, hadithi za historia, hadithi za opera. Sanamu za maua ya siagi ni za aina mbalimbali kama vile jua, mwezi, nyota na sayari, maua, miti, ndege , wanyama, vibanda na majumba na sanamu mbalimbali za mabuddha na mababu, Majemedari na watu mashuhuri. Sanamu hizo zilichongwa vizuri na kuonesha sura halisi ya kupendeza, ambazo ni vitu vya sanaa vya kiwango cha juu.

Sanamu ndogo ndogo za maua ya siagi zilizochongwa vizuri na kupakwa rangi ya kupendeza huchukuliwa kama sadaka za kutambika, aina zake mbalimbali zinaonekana ishara ya heri na baraka. Na sanamu nyingine za maua ya siagi huwekwa kwa pamoja ambazo zinawavuta watu kwa mitindo yao ya kufurahisha.

Opera ya kitibet

Opera ya kitibet ina historia ndefu tangu enzi na dahari, mitindo ya opera hiyo ni ya aina mbalimbali. Michezo ya Opera ya kitibet kama vile "Binti wa mfalme Wencheng" na "Mwana wa Mfalme Nosang" imekuwa michezo inayosifiwa na kupendwa na watu kwa miaka mingi tangu zamani, muziki wa michezo hiyo ni mwororo sana, vifuniko vya nyuso na mapambo ya nguo ya wahusika wa michezo hiyo ni ya rangi mbalimbali na kupendeza kiajabu. Yote hayo yameonesha msingi imara wa utamaduni kwenye opera ya kitibet.

Opera ya kitibet ni michezo ya sanaa inayoonesha nyimbo na ngoma za kienyeji. Toka karne ya 15, mtawa Tangdongjiebu wa madhehebu ya Geju alitunga michezo ya opera ya kitibet na kuongoza wachezaji kuonesha michezo ya nyimbo na ngoma iliyoeleza hadithi fupi katika sehemu mbalimbali. Baada ya miaka mingi, michezo ya opera ya kitibet imeendelea vizuri, michezo yenyewe ilitungwa kikamilifu na kusimulia hadithi nzuri na kuongeza vivutio mbalimbali pamoja na mapambo, mitindo tofauti ya uimbaji kwa kufuata bendi na uimbaji wa wanaoambatana, opera ya kitibet kweli ni michezo mbalimbali ya sanaa.

Watibet wanapenda sana michezo ya opera ya kitibet, kila yanapofanyika maonesho ya michezo ya opera hiyo, watu wengi kutoka sehemu za mbali hata wanaweza kumiminikia kwenye uwanja mmoja kutazama maonesho.


1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13