11: Mikoa ya Xinjiang na Tibet

Uchumi wa Xinjiang

Kazi za Viwanda za Xingjiang

Hivi sasa uchumi wa viwanda mkoani Xinjiang umekuwa na ongezeko la kasi, Xinjiang imekuwa na mfumo kamili wa kazi za viwanda zikiwa ni pamoja na chuma, chuma cha pua, makaa ya mawe, mafuta ya asili ya petroli, mitambo, kemikali, vifaa vya ujenzi, nguo, sukari, karatasi, ngozi na sigara. Kwa kutumia hali bora ya rasilimali za mkoa huo, Xinjiang imeanzisha sekta za uzalishaji mali wenye umaalumu wa Xinjiang. Hivi sasa, Xinjiang imekuwa na viwanda zaidi ya elfu 60 vya aina mbalimbali vya kazi za usafishaji wa mafuta ya asili ya petroli, makaa ya mawe, uyeyushaji wa madini, umeme, nguo, kemikali, mitambo, vifaa vya ujenzi na chakula, ambavyo vinazalisha bidhaa za aina zaidi ya 2,000.

Kilimo cha Xinjiang

Xinjiang ina mwangaza mwingi wa jua pamoja na ardhi kubwa. Wakazi wa huko wameendeleza kilimo kwenye sehemu zenye maji. Mazao ya kilimo ya Xinjiang ni pamoja na ngano, mahindi na mpunga. Mazao ya kiuchumi ni pamoja na pamba, mboga za kutengenezea sukari na maua ya kutengenezea bia. Kati ya mazao hayo ya kilimo, uzalishaji wa pamba unachukua nafasi muhimu nchini China, tena pamba hiyo ina nyuzi ndefu, ambazo ubora wake unalingana na pamba maarufu za Misri.

Xinjiang pia inajulikana kwa uzalishaji wa matunda na matikiti ya aina mbalimbali yakiwemo zabibu, matikiti ya Hami, matikiti ya maji, matufaha, mapea, mapichi, mapera, maaprokoti na matunda mengine, lakini zabibu na matikiti ya Hami ni matamu sana. Katika miaka ya karibuni kilimo cha Xinjiang kimeendelezwa kuwa kwa haraka na kuwa sekta kubwa yenye kazi za uzalishaji na usindikaji.

Mifugo ya Xinjiang

Xinjiang ina mifugo ya aina nyingi na ni moja ya sehemu muhimu ya ufugaji. Toka zamani, Xingjian ni sehemu inayozalisha farasi bora na wanyama wengine kama ng'ombe, kondoo, punda ngamia na yak. Uzalishaji wa nyama ya kondoo wa Xinjiang unachukua nafasi ya pili nchini China, idadi ya mifugo ni zaidi ya milioni 40.

Eneo la mbuga ya malisho yenye majani mkoani Xinjiang ni kilomita kiasi cha elfu 570 ikichukua 87% ya maeneo ya kilimo, misitu na malisho ya mifugo. Rasilimali ya malisho yenye majani ni muhimu ya na ya kimsingi kwa uendelezaji wa ufugaji wa mifugo mkoani Xinjiang, ambayo kiasi cha 70% ya mifugo ya Xinjiang inategemea majani yake. Xinjiang ni kituo cha uzalishaji wa aina bora na mpya za mifugo nchini China.

Kilimo chenye Umaalumu wa Xinjiang

Kilimo chenye umaalumu wa Xinjiang ni pamoja na sekta zaidi ya kumi zikiwemo za utengenezaji wa pombe, vinywaji, maziwa, vitu vya kemikali vinavyotumika kila siku kwenye masiha ya watu, manukato, sukari, vitu vinavyotumiwa na wakazi wa huko na usindikaji wa vito.


1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13