11: Mikoa ya Xinjiang na Tibet

Dini ya Xinjiang

Mahali Penye Dini za Aina Nyingi

Xinjiang ni mahali pekee duniani penye aina nne kubwa za dini ya kibudha, kijing, kimoni na kiislam. Mnamo karne ya kwanza, dini ya kibudha ilienezwa hadi sehemu ya mashariki kwa kufuata njia ya hariri na kufikia sehemu nyingi za China. Dini ya kijing ni dhahebu moja la dini ya kikristu, ambalo liliingia Xinjiang katika karne ya 6. Utafiti uliofanywa kuhusu mambo ya kale unaonesha kuwa dini ya kijing ilienea sana huko Xinjiang, na kuwa moja ya kituo cha dini hiyo, isipokuwa ilianza kufifia baada ya dini ya kiislam kuingia huko hapo baadaye. Katikati ya karne ya 10, dini ya kiislam iliingia Kashi kwa kufuata njia ya hariri, na ilienea sana kwenye sehemu ya Xinjiang kati ya karne ya 16 hadi karne ya 17. Hivi sasa wengi wa watu wa makabila kumi ya Xinjiang ni waumini wa dini ya kiislam.

Waumini wa Dini wa Xinjiang

Hadi hivi sasa, Xinjiang bado ni sehemu yenye aina nyingi za dini, ambayo dini ya kiislam ina athari kubwa zaidi katika shughuli za jamii. Katika sehemu ya Xinjiang kuna mahali zaidi ya 23,000 pa kufanyia shughuli za kidini, ambapo ni pamoja na misikiti, mahekalu ya Kilama na makanisa.

Katika sehemu ya Xinjiang watu wa makabila 10 yakiwemo ya waurgur, wakazakstan na wahui ni waumini wa dini, idadi ya waumini wa dini wamezidi milioni 9 ikichukua 56.3% ya jumla ya idadi ya wakazi wa Xinjiang.

Idadi ya watu wa kabila la wamongolia wanaoishi mkoani Xinjiang inakaribia elfu 80, watu wa kabila hilo ni waumini wa dini ya kibudha ya kitibet, katika sehemu hiyo kuna mahekalu ya kibudha 49. Sehemu ya Xinjian kuna wakristu karibu elfu 30 na makanisa 24. Idadi ya wakatoliki katika sehemu ya Xinjiang imezidi elfu 4 pamoja na makanisa na mahali pa kufanyika shughuli za kidini 25. Mbali na hayo, Xinjiang ina watu wa kabila la warusi zaidi ya 100 ambao ni waumini wa dhahebu la Orthodox pamoja na makanisa mawili.


1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13