Uchumi wa Tibet
VIWANDA
Hapo zamani Tibet ilikuwa na karakana za ufundi wa jadi wa kutengenezea mazulia, vitambaa vya sufu, apron, viatu, bakuli za mbao na vitu vingine vidogo vidogo. Baada ya Tibet kukombolewa kwa njia ya amani mwaka 1951, hususan baada ya kufanya mageuzi ya demokrasia mwaka 1959, vilijengwa viwanda vingi vya uzalishaji wa umeme, uyeyushaji madini, uchimbaji wa makaa ya mawe, mitambo, kemikali, vifaa vya ujenzi, viwanda vya kazi kuhusu misitu, viberiti, plastiki, nguo, chakula, ngozi na karatasi.
Mwaka 2003, pato la viwanda vya Tibet lilifikia Yuan za Renminbi bilioni 1.8, kiasi hiki kilichukua 15% ya jumla ya pato la Tibet. Katika siku za baadaye Tibet itaendeleza kazi za viwanda, kurekebisha muundo wa uzalishaji mali, na kujitahidi kuendeleza matumizi ya raslimali za aina tatu za madini, misitu na mazao ya mifugo, licha ya hayo itaendeleza mageuzi ya teknolojia ya viwanda na kuongeza pato la viwanda.
KILIMO
Ufugaji unachukua nafasi muhimu katika sekta ya uzalishaji wa kilimo mkoani Tibet. Uzalishaji wa mazao ya kilimo uko katika sehemu yenye mabonde, zao kuu la kilimo ni shayiri ya uwanda wa juu ikifuatwa na mazao mengine ya ngano, chakula cha mifugo, njegere pamoja na mazao kidogo ya mpunga na mihindi.
Ufugaji
Ufugaji ni njia muhimu ya uchumi mkoani Tibet, na u na historia ndefu na una nafasi kubwa ya kuendelea zaidi. Hivi sasa kuna mbuga za majani zenye ukubwa karibu hekta milioni 82, kati ya eneo hilo mbuga zinazoweza kutumika kwa ajili ya malisho ni hekta milioni 56, kiasi ambacho moja kwa tano ya malisho yote nchini China na ni moja ya sehemu tano kubwa za ufugaji nchini China.
Ufugaji unachukua 60% ya uchumi wa Tibet, wanyama wanaofungwa ni nyati na kondoo. Wanyama hao ni wa kabila la Tibet, ambao wanasifa ya kuvumilia baridi na ukame.
Misitu
Mkoani Tibet kuna misitu yenye maeneo hekta milioni 6.3 ambayo ni 5% ya ardhi yote ya mkoa. Misitu hiyo ni akiba ya magogo yenye ujazo wa mita bilioni 1.4, ambayo inachukua nafasi ya pili nchini China. Miti mingi katika misitu hiyo ni misonobari ambayo ina sifa ya kukua haraka. Mkoa wa Tibet unatilia maanani sana hifadhi ya mazingira. Sehemu 18 za hifadhi mazingira zimeanzishwa ambazo ni asilimia 33.9 ya ardhi yote ya Tibet.
Mradi wa Kuusaidia Mkoa Tibet
Mkoa Tibet ambao unajulikana kama ni paa la dunia uko nyuma kiuchumi kutokana na sababu za kihistoria na mazingira ya kimaumbile. Mwaka 1994 serikali kuu ilifanya mazungumzo ya mara ya tatu na inaanzisha mradi wa kuusaidia Mkoa Tibet, mradi huo unahusu, ufugaji, misitu, nishati, mawasiliano, mawasiliano ya posta, jumla unahitaji yuan bilioni 4.86. hivi sasa mradi huo umekamilika na kuanza kutoa mchango mkubwa.
Msaada wa Mkoa Tibet umesaidia kuboresha maisha ya watu wa Tibet. Mjini Lhasa wenyeji wanaweza kuangalia TV, majumba ya ghorofa yamejengwa badala ya zile nyumba za chini za zamani, watoto wa wakulima wanaokwenda shule, bendera za rangi mbalimbali zinapepea mbele ya Kasri la Potala zikiwavutia watalii kwa mwaka mzima.
|