21: Uchoraji wa Jadi

Vitu vya kuchezea kwa watoto

Vivuli vya Picha Zilizotengenezwa kwa Ngozi (1)

Mchezo wa vivuli vya picha zilizotengenezwa kwa ngozi ni aina moja ya michezo ya sanaa inayopenswa na Wachina, mchezo huo umeenea zaidi katika sehemu ya kaskazini magharibi ya China.

Mchezo huo ulikuwa unachezwa sana katika Enzi ya Ming na Enzi ya Qing (karne ya 14 – 19).

Picha za ngozi zinatengenezwa kwa ngozi ya ng'ombe mdogo mweusi, ngozi hiyo huwa laini na si nene wala nyembamba. Baada ya kuondoa manyoya na kukaushwa, ngozi hiyo inaweza kutumiwa kutengeneza picha. Kwanza picha inachorwa kwenye ngozi na kisha inakatwa na kuchongwa kwa mujibu wa picha iliyochorwa, baadaye picha inapigwa pasi baada ya kutiwa rangi ambayo inaweza kupitisha mwangaza. Baada ya picha zote zinazohitajika katika mchezo zinapangwa pamoja. Wakati huo mchezo wa vivuli vya picha zilizotengenezwa kwa ngozi unaweza kuchezwa. Mchezo huo unachezwa kwa vivuli vya picha kwenye pazia, vivuli hivyo vinatokea kutokana na mwangaza wa taa unaokuwa nyuma ya picha.

Kwenye upande wa kushoto wa picha ni mungu wa dini ya Dao, na kwenye upande wa kulia ni picha ya Mencius.

Mchezo huo unachezwa na huku wachezaji wanaimba kwa sauti ya juu. Kila sehemu ya picha, miguu, mikono, kichwa inaweza kucheza. Ni mchezo unaowavutia sana wenyeji.

Michezo ya vivuli vya picha zilizotengenezwa kwa ngozi huonesha hadithi za historia.

Vivuli vya Picha Zilizotengenezwa kwa Ngozi (2)

Mchezo wa vivuli vya picha za ngozi ni mwanzo wa aina nyingi za michezo kienyeji katika sehemu ya kaskazini magharibi ya China.

Picha zilizochongwa kwa ngozi huwa ni rahisi lakini hazipotezi sura muhimu za wahusika, wausika tofauti katika hadithi, sura na mavazi pia ni tofauti kwa ajili ya kuonesha hulka za wahusika tofauti. (Picha: Kusafiri)

Picha ya "Kusafiri" (ya kwanza kushoto) mhusika anajitokeza zaidi kwa nafasi yake, rangi yake na sura yake jinsi anavyokaa.

Vivuli vya Picha Zilizotengenezwa kwa Ngozi (3)

Picha za ngozi zilizochongwa mkoani Shanxi hupakwa rangi wazi nyekundu, kijani, na manjano, na picha hizo hazibadiliki wala kuozwa.

Watu wanaoashiria baraka katika enzi za kale za China hutokea katika michezo ya vivuli vya picha zilizotengenezwa kwa ngozi mkoani Shanxi.

Picha ya "Msichana Anayepodoa" inaonesha msichana akijipamba mbele ya kioo. Wakati wa kuonesha picha hiyo ya msichana pia kuna picha za meza, kiti, sanduku na kabati ambazo zote ni za mtindo wa kale.

Vitu vya Udongo vya Kuchezea Watoto (1)

Mkoani Henan kuna mila ya kutengeneza vitu vya udongo vya kuchezea watoto. Vitu hivyo huwa ni "kima anayejishika magoti", "kima mwenye sura ya mtu", "kima anayempakata mtoto wake", n.k.

Vitu hivyo sivyo tena vitu vya kuchezea watoto, bali ni aina moja ya sanaa kutokana na historia ndefu. Vitu hivyo hufinyangwa kwa udongo, kwenye mgondo au chini kuna kitundu ambacho kikipulizwa kinaweza kutoa sauti. Kima huyo amefinyangwa kwa kupiga chuku, anaonekana kama kima na pia kama binadamu mwenye uso wa mviringo, macho ya duara kama gololi.

Vitu vya Kuchezea Watoto (2)

Vitu vya udongo vya kuchezea watoto katika sehemu ya Huaiyang mkoani Henan huwa ni ndege au mnyama mwenye vichwa viwili. Baada ya kufinyangwa na kukaushwa, hupakwa rangi na kuchorwa sura ya kitu chenyewe.

Kwenye picha, sura ya nguruwe ni ya ajabu, nguruwe mmoja anakaa juu ya mwingine, rangi nyeupe inatawala, masikio na vina ukubwa tofauti. Ni kitu cha kuchekesha.

Vitu vya Udongo vya Kuchezea Watoto (3)

Vitu vya udongo vya kuchezea watoto wilayani Zun vinapatikana tu katika sikukuu za kienyeji. Kwenye gulio vitu hivyo, ambavyo vinaweza kutoa sauti baada ya kupulizwa huuzwa.

Vitu hivyo hupakwa rangi nyekundu, manjano na nyeupe. Vitu hivyo huwa ni picha za watu wanaosimuliwa katika hadithi za enzi za kale.

Sanamu zilizofinyangwa huwa ni watu katika hadithi za mapokeo ambao watu wanapoona jinsi sanamu zilivyo hukumbuka hadithi zenyewe.

Vitu vya Udongo vya Kuchezea Watoto (4)

Vitu vya udongo vya kuchezea kwa watoto katika wilaya ya Zun mkoani Henan huwa ni wanyama na ndege, hasa farasi na watu wanaosimuliwa katika hadithi za kale.

Sanamu hizi zinazofinyangwa zina sura na rangi mbalimbali. Kutokana na kuwa watu tofauti, sanamu zao na mavazi yao pia ni tofauti.

Vitu vya Udongo vya Kuchezea Watoto (5)

Jogoo la udongo lililofinyangwa wilayani Xincheng linajulikana sana. Majogoo ya udongo wamegawanyika ukubwa wa aina tatu, yaani kubwa, kiasi na ndogo. Kubwa kabisa ina kimo cha senti mita 25, na ndogo ina kimo sentimita 6.

Jogoo la udongo hupakwa rangi nyekundu kwenye kilemba, rangi nyeusi kwenye shingo, na mkia ulioinuka unaonesha ujeuri wake.

Vyombo vya Udongo vya Kuchezea Watoto (6)

Katika historia ya China, mji mdogo wa Baizhen wilayani Xincheng ulikuwa ni kama maskani ya vyombo vya udongo vya kuchezea watoto. Sanamu nyingi zilizofinyangwa ni za watoto au watu wanaosimuliwa katika masimulizi ya kale.

Sanamu ya mpanda farasi mwenye upanga ni sanamu kwa ajili ya pambo la chumbani. Inasemekana kuwa sanamu hiyo inaweza kulinda usalama na kuondoa bahati mbaya nyumbani.

Rangi muhimu iliyopakwa kwenye sanamu kama hiyo ni nyekundu na manjano.

Kikaragosi Kinachochezeshwa kwa Vijiti

Vikaragosi hivyo pia vinaitwa "vibaraka vinavyochezeshwa kwa vijiti". Vikragosi katika picha hizo vimechongwa kwa mbao, na macho yake yanaweza kucheza. Vikaragosi hivyo vinagawanyika katika saizi za aina tatu, yaani kubwa, ya katikati na ndogo.

Kikaragosi huwa na mitindo tofauti kutoka na sehemu tofauti. Lakini sura za vikaragosi huambatana na opera za jadi za kienyeji. Vikaragosi vilivyotengenezwa katika sehemu tofauti pia zina tabia tofauti na zinavutia kwa sifa tofauti.

Vitu vya Kuchezea Watoto Vilivyotariziwa

Vitu vya kuchezea Watoto Vilivyotariziwa hupatikana katika sehemu ya kaskazini magharibi ya China. Vitu hivyo huwa ni samaki, ndege, chura, kichwa cha nguruwe, wadudu, simba. Vitu hivyo vimeonesha matumaini mema ya wakulima Kwa maisha.

Katika picha, ndege aliyening'inizwa ametariziwa kwa makini na kwa nyuzi za rangi mbalimbali kwa mujibu wa jinsi wanavyofikiri watarizi.

Vyombo vya Kuchezea Watoto "Mfalme Kima"

Katika uchoraji wa jadi sura za "mfalme kima" katika hadithi za "Safari ya Kwenda Magharibi" zinachorwa sana. Vitu vya kuchezea watoto huonesha jinsi kima anavyokuwa mwepesi wa kucheza na wa akili.

Katika picha mfalme kima na mwenzake nguruwe wanaonekana wazi kwa tabia zao, mmoja mwepesi mwingine mpole na mwenye sura mbaya. Sanamu ya mfalme kima inaonesha kima mwepesi wa kuruka na kukimbia na kuparamia miti, na sanamu ya nguruwe inaonesha tabia yake ya uvivu.

Uchongaji kwenye Tunguri

Wasanii wa kienyeji huchonga picha kwenye tunguri, wanatumia kisu kidogo kuchonga picha na kisha wanapaka masizi, na baadaye kuyaondoa mistari iliyochongwa inabaki myeusi, na picha ikaonekana.

Picha kwenye tunguri huwa ni maua au sura za watu waliokuwa katika hadithi za kale.

Kikaragosi cha Pembua Nafaka

Kikaragosi cha kupembua nafaka ni aina nyingine ya vitu vya kuchezea watoto. Kikaragosi hicho kinaweza kucheza kwa kuvuta nyuzi zilizofungwa kwenye kila kiungo.

Kikaragosi hicho ni kama mtu anayepembua nafaka, kichwa na mwili ni kitu kimoja ila mikono na miguu inaunganishwa kwa nyuzi za chuma, nyuzi zikivutwa mikono na miguu hucheza cheza. Rangi ya kikaragosi ni ya aina mbalimbali.

Sanamu za Mbao

Katika mkoa wa Shandong kuna sanamu ya mtu iliyochongwa kwa mbao, ndani sanamu hiyo iko wazi.

Sanamu hiyo ni mwili wa mtu kuchongwa mikono wala miguu, ndani yake hutiwa mchanga, sanamu inapozungushwa hulialia. Sanamu hiyo hupakwa rangi za kuwavutia watoto, na inapozungushwa inalialia.

Tiara

Tiara ni moja ya vitu vinavyotumiwa na watu. Kurusha tiara pia kunamaanisha kufukuza "kisirani". Kurusha tiara licha ya kuweza kujifurahisha, pia inaweza kujenga afya, na mchezo huo unaenea zaidi katika sehemu za Weifang, Beijing, Tianjin na Nantong mkoani Jiangsu.

Mkoa wa Shangdong una historia ndefu ya kuchora picha kwenye tiara kama picha za mwaka mpya. Mchezo wa kurusha tiara unachezwa sana katika miji ya Weifang mkoani Shandong, Beijing na Tianjin na mji wa Nantong mkoani Jiangsu. Uchoraji wa picha kwenye tiara mjini Weifang una historia ya ndefu sana. Picha za huko zina mtindo wazi wa kienyeji.

Tiara za Beijing zina historia ya miaka 300, tiara za Beijing hutengenezwa kwa umbo la ndege na popo. Katika picha ni tiara ya ndege mbayuwayu wawili, mmoja wa rangi ya buluu, na mwingine wa rangi nyekundu, ikionesha "mume na mke wanashindana kuruka juu".

Opera ya Nuo

Opera ya Nuo ina historia ndefu. Opera hiyo ilianzia kufanya matambiko, na ilipokuwa katika Enzi ya Shang (1600 K.K.-1046 K.K.) ilikuwa ni aina ya kufukuza mashetani.

Wachezaji wa opera hiyo huvaa vinyago usoni wakiiga mashetani wa aina mbalimbali.

Katika sehemu ya kaskazini ya mkoa wa Guizhou mpaka sasa bado opera hiyo inachezwa. Wachezaji huwa kiasi cha mia moja wakivaa vinyago vya aina mbalimbali.

Vinyago huchongwa kwa mbao, ambavyo huchongwa kwa sura za kutisha, baadhi vinyago vina pembe, baadhi vina meno marefu, baadhi vina midomo mikubwa, na baadhi macho yanajitokeza sana na nyusi nene nyeusi, vinyago hivyo vinatisha kwa sura.

Opera ya Di

Opera ya Di inachezwa sana katika mkoa wa Guizhou. Kila katika sikukuu za Kichina, opera hiyo huchezwa. Wachezaji huvaa vinyago vya aina mbalimbali wakionesha wahusika mbalimbali katika hadithi za mapokeo.

Waigizaji katika opera hiyo wanagawanyika katika jemadari, ofisa, jemadari kijana, jemadari mzee na jemadari mwanamke. Wanawake wanapocheza huvaa vinyago vyenye mayoya ya tausi au vyenye michoro ya kipepeo na nyuki.

Pichani, jemadari ana paji pana, nyusi nene na kuinuka, pua pana na macho makubwa ya kujitokeza, na anaonekana mkali.


1 2 3 4 5 6