21: Uchoraji wa Jadi

Mapambo kwenye nguo

Kitambaa cha Mabegani

Kitambaa cha mabegani kilianzia Enzi ya Sui (581-618) na ilipofika Enzi ya Qing (1644-1911) kitambaa hicho kilikuwa pambo, hasa kwa wanawake. Kitambaa hicho kinatariziwa kwa muda mrefu, na picha kwenye kitambaa hicho huwa ni maua, ndege au watu katika hadithi za mapokeo. Kitambaa cha mabegani katika picha ni cha mkoa wa Henan, picha iliyotariziwa ni mawingu, maua na ndege na watu na daraja.

Viatu Vilivyotariziwa vya Kabila la Wayi

Mapambo kwenye mavazi ya kabila la Wayi kusini magharibi mwa China, licha ya kutia uzuri mavazi pia yanaonesha ngazi ya watu, umri na itikadi ya kabila hilo. Mapambo hayo yanatofautiana kwa aina za maua na sehemu za kutarizi mapambo hayo kwenye mavazi.

Pichani, viatu vilivyotariziwa ni vya mwanamke, vinaonekana kama mashua mbili ndogo. Viatu hivyo huvaliwa na bibi harusi anapokwenda kwa bwana harusi, ili awe salama njiani.

Mkoba wa Pambo

Mkoba wa pambo ni aina moja ya vitu vya sanaa nchini China. Mkoba huo ni pambo na pia unaweza kutiwa vitu vidogo ndani, na mara nyingi hutiwa vitu vya manukato. Kulikuwa na aina nyingi za mifuko hiyo, kama vile popo, chenza, chura n.k..

Pichani mkoba una umbo la chura, na umetariziwa kwa makini. Baadhi ya mikoba hushonwa picha za wanyama wa aina 12 wanaowakilisha miaka 12.

Utarizi wa Wilaya ya Linfen Mkoani Shanxi

Utarizi katika wilaya ya Linfen ya Mkoa wa Shanxi, kaskazini mwa China umeenea sana. Watu wana tabia kutarizi nguo kwenye kola, sketi, mito ya kulalia, vitambaa vya mezani n.k. Picha za kutariziwa huwa ni ndege, miti, korongo au watu wanaosimuliwa kwenye hadithi za kale.

Pichani ni dragoni wawili wanaocheza lulu. Dragoni wawili wanaonekana wenye nguvu, na vitu vilivyopamba kwenye picha hiyo ni mawimbi ya maji, popo, miungu.

Mapambo kwenye Mavazi ya Kabila la Wayao

Wayao wanaishi sehemu ya kusini ya China, kuna aina zaidi ya 60 za mapambao hayo.

Mapambo ya mavazi hutariziwa kwenye sehemu ya kiuno, miguu ya suruali na kifuani, na baadhi hutiwa kwenye aproni. Mapambo hayo yameonesha mikono hodari wa kabila la Wayao.

Utarizi wa Kabila la Wamiao

Katika mkoa wa Guizhou wanaishi Wamiao wengi, watu hao wana mila ya kutarizi mapambo kwenye nguo. Vitu wanavyovitarizi huwa ni dragoni, ndege, samaki, maua, vipepeo na tandu.

Pichani ni aproni iliyotariziwa kwa vipepeo, tandu kwa nyuzi za rangi mbalimbali. Pambo linalotariziwa kwenye nguo mara nyingi huwa mtu anayepanda dragoni, ikionesha ujasiri na ushupavu wa Wamiao. Kadhalika, pia kuna picha za tarizi za swala, na wanyama wa aina nyingi.

Kitambaa Kilichochapwa kwa Maua ya Buluu

Kitambaa kilichochapwa kwa maua ya buluu kinawavutia sana Wachina. Kitambaa hicho ni cha pamba na kinatumia aina moja ya mimea ili kupata rangi ya buluu, na rangi hiyo haichujuki na haina madhara kwa afya. Kitambaa hicho hutumika kushona nguo, pazia la mlango, chandarua na kitambaa cha kufungia nguo.

Kitambaa hicho pia kinawavutia wageni kwa ajili ya kushonea nguo.

Aproni

Aproni pia ni aina moja ya mapambo ya nguo kwa wanawake, sehemu ya chini ya aproni ni nusu duara, au ya ncha.

Kwenye aproni kuna maua ya kuchapwa au ya kutariziwa, na vitu vinavyotariziwa huwa ni ndege, maua, chura, mayungiyungi, wadudu, majani na picha nyingine ambazo zote zinaonesha matumaini mema na baraka.

Pichani, rangi kuu ya aproni ni ya kijani na imetariziwa watu wanaosimuliwa katika hadithi za kale na maua.

"Kufuli la Maisha Marefu" Linalovaliwa Shingoni

Kufuli la maisha marefu ni kitu cha kuomba baraka kwa watoto wa kiume na wa kike. Kufuli hilo hufungwa kwa mkufu na kuvaliwa shingoni mpaka watoto wanapooa au kuolewa.

Hapo zamani kutokana na hali ya matibabu kuwa duni, watoto walikuwa wanakuwa wakiwa bado wadogo, kwa hiyo wazazi waliwalisha watoto wao "kufuli la maisha marefu" shingoni ili wapate maisha marefu.

Kwenye kufuli kuna michongo au maneno ambayo yote yanaonesha ombi la maisha marefu na baraka.

Mapambo Yaliyotariziwa kwenye Mavazi ya Kabila la Wabai

Mkoani Yunnan kuna makabila madogo madogo zaidi ya 20, na kila kabila lina mila ya kutarizi mapambo kwenye mavazi yao. Utarizi huo umekuwa na miaka zaidi ya elfu mbili. Utarizi wa kabila la Wabai huonekana kwenye shela, aproni, kofia kubwa ya ukili na viatu.

Pichani: Wasichana wa kabila la Wabai hufunga nywele kwa utepe mwekundu kwa kuonesha kuwa hawajaolewa na kufunga sketi kwa utepe uliotariziwa.

Kitambaa cha Soli Kilichotiwa Ndani ya Viatu

Wachina wana mila ya kutarizi maua kwenye kitambaa cha soli ndani ya viatu, maua hayo yanaonesha matumaini mema ya mtu aliyemtarizia.

Pichani ni vitambaa vya soli vilivyotariziwa na mama mkwe kwa ajili ya mkamwana. Rangi nyekundu inamaanisha furaha, na matunda yanamaanisha atapata watoto wengi. Vitambaa hivyo hutumika wakati wa ndoa kwa kujitakia baraka.

Nguo Yenye Vipande Vingi vya Kitambaa

Nguo hiyo inatokana na mila ya zamani ambayo watoto wanakua na afya kwa kutegemea msaada wa chakula na nguo kutoka kwenye familia mbalimbali.

Nguo yenye vipande vingi vya kitambaa inamaanisha nguo inapatikana kutoka familia mbalimbali. Nguo hiyo ina rangi mbalimbali kutokana na vitambaa tofauti. Licha ya nguo za aina hiyo pia kuna fulana. Watu wa sehemu ya kaskazini wa mikoa ya Shan'xi, Shanxi, Gansu, Henan, Hebei na Shandong wana desturi ya kuvaa nguo hizo.

Mfuko wa Kiunoni

Mfuko wa kiunoni ni aina moja ya pambo kwenye kiuno, maumbo ya mfuko yalikuwa ni ya aina mbalimbali, kama duara, mraba, ya mstatili n.k. Picha za vitu vinavyoshonwa kwenye mfuko huo huwa ni maua, ndege na wanyama, ambavyo vinaonesha matumaini mema ya mtu aliyeshona.

Michoro kwenye mikoba pia huanbatana na maneno yakimaanisha matumaini mema na mustakbali mzuri kwa watu wanaotumia mikoba hiyo

Pichani, mfuko huo una umbo la tunguri, na kwenye shindo ya tunguri hilo kuna mashuke ya dhahabu, na kwenye mbele na nyuma kuna maneno "Uwe mnyekekevu wakati wote".


1 2 3 4 5 6