• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Barua za wasikilizaji 0120

    (GMT+08:00) 2009-01-22 16:48:29

    Msikilizaji wetu "Francis Njuguna" osnjuguna@yahoo.com -Nairobi, Kenya ametoa maoni yake kwenye tovuti yetu ya mtandao wa internet kwa kusema kuwa anaandika ili apate kuitakia Radio China Kimataifa kila aina ya heri na fanaka katika kipindi hiki cha mwaka huu mpya wa 2009, anasema hakika radio hii tuipendayo imepata kufanya mengi katika vipindi vya hapo nyuma na ni matumaini yetu ya kwamba itaendelea kufanya mengi katika kipindi hiki cha mwaka huu mpya kwa kila njia

    Mungu aibariki Redio China Kimataifa ili ipate kuhudumia watu wote ulimwenguni ambapo lugha hii ya kiswahilim inatumika

    Gasto Francis Mkawe P. O. Box 11091, Arusha, Tanzania anuani yake kwenye mtandao wa internet ni "eunice adema" eunadema@yahoo.com anasema nakupongezeni sana wafanyakazi wote wa CRI. Naomba mjiunge katika masafa mafupi ya FM ili hata sisi wa Tanzania tuwasikie vyema. Naomba mnitumie kalenda na vipeperushi vyenu. Asante sana

    Eunice Adema Manyengo [Cool Lady]' S.L.P 22 Kitale-Kenya.

    yeye anapongeza Radio China Kimataifa kwa matangazo yao,pamoja na vipindi vyao ikiwamo jifunze kichina. nikiwa shabiki sugu wa radio china naomba mnitumie kadi za salamu za radio china pamoja na vitabu vya kujifunza lugha ya kichina. pia naomba urafiki wa raia wa nchi ya china tuwe tukiwasiliana naye mara kwa mara,hata ifike siku nije nitembee nchini china. ahsanteni sana na mungu wa amani awabariki kwa vile tumeanza mwaka mpya uwe wa mafanikio kwa ulimwengu kwa jumla.

    Mchana J. Mchana wa sanduku la posta 1878 Morogoro Tanzania ametoa maoni yake kwenye tuvuti yetu ya mtandao wa internet akisema,kwanza nawatakia heri ya mwaka mpya viongozi, watangazaji, waandishi wa habari wa Radio China Kimataifa bila kuwasahau watangazaji wa radio KBC kwani kwa sasa tunao pamoja na kwangu mimi kama mchana j.mchana nawaona ni ndugu zangu wa karibu wakiongozwa na Omunga Kabisayi kwani tunashirikiana vizuri sana hasa kupitia salamu za KBC usiku.


    1 2 3 4 5 6 7 8
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako