• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Barua za wasikilizaji 0120

    (GMT+08:00) 2009-01-22 16:48:29

    Namna ya kujikinga na homa ya mafua ya ndege ni suala linalofuatiliwa sana. Mtafiti wa kituo cha kinga na udhibiti wa magonjwa cha China Bw. Wang Jian alisema: Sauti 4

    "maambukizi ya maradhi yanaundwa na pande tatu, yaani chanzo cha kuambukiza, njia za kuambukiza na watu ambao ni rahisi kuambukizwa maradhi hayo. chanzo cha kuambukiza cha homa ya mafua ya ndege ni ndege walioambukizwa virusi vya ugonjwa huu, njia ya kuambukiza kwake ni kwa kugusana, sisi sote ni rahisi kuambukizwa ugonjwa huo, kwa kuwa bado hakuna chanjo inayotumika kwa watu wengi. Moja kati ya pande hizo tatu ikikatika maambukizi ya ugonjwa huo yatazuiliwa. Kwa sasa tunaloweza kufanya ni kukata njia za kuambukiza."

    Wataalamu wanasema, kwa kukata njia za kuambukiza tunapaswa kuepusha kugusana na ndege mbalimbali, kama tukigusana na ndege na kinyesi chao, tunapaswa kunawa mikono mara moja.

    Wataalamu pia wanapendekeza kuwa mbinu nzuri ya kujikinga dhidi ya homa ya mafua ya ndege ni kuongeza kinga ya mwili, kupata usingizi wa kutosha, kula chakula kwa uwiano pamoja na kufanya mazoezi kwa kiasi mwafaka, pia tunapaswa kuwa na mwenendo mzuri wa maisha n.k.


    1 2 3 4 5 6 7 8
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako