• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mji wa Qingdao wa mkoa wa Shandong

    (GMT+08:00) 2009-02-16 16:42:24

    Mandhari ya mji wa Qingdao ni nzuri sana kwa kuwa mji huo uko chini ya milima na kwenye kando ya bahari, tena hali ya hewa ya huko ni nzuri pia. Licha ya kutazama mandhari ya bahari, kupanda milima na kula vyakula vya baharini, hivi sasa kuna sehemu moja yenye vivutio iitwayo "Ua wa Kuni" kwenye mtaa wa kale wenye historia ya zaidi ya miaka 100. Huko, watu licha ya kuweza kupata nafasi ya kula aina mbalimbali za vyakula vya jadi, wanaweza kuburudika kwa maonesho ya michezo ya jadi ya China, zikiwemo opera ya Beijing na opera ya Dagu.

    "Ua wa Kuni" uko kwenye sehemu yenye shughuli nyingi za biashara iliyoko mtaa wa Zhongshan mjini Qingdao. Inasemekana, sehemu hiyo ilikuwa ni soko la kuni hapo zamani, ziliuzwa kuni kwenye mtaa huo mzima, tokea kipindi cha kati ya miaka ya 20 ya karne iliyopita, sehemu hiyo pamoja na mtaa wa Jiangning zilijulikana kutokana na "Ua wa Kuni". Mjumbe wa kamati ya wataalamu ya hifadhi ya mabaki ya utamaduni ya Qingdao, Bw. Wang Duo alisema, sababu ya "Ua wa Kuni" kuitwa mtaa wa Jiangning ni kuwa Jiangning ilikuwa jila la zamani la mji wa Nanjing wa mkoa wa Jiangsu, mtindo wa jengo la "Ua wa Kuni" ni sawa na ule mtindo wa majengo ya wakazi na maduka ya Jiangsu, hivyo mtaa huo unaitwa kuwa ni Jiangning. Bw. Wang Duo alisema, katika miaka ya 30 ya karne iliyopita, "Ua wa Kuni" ni mahali penye shughuli nyingi zaidi katika mji wa Qingdao, ambapo watu waliweza kupata vyakula vya aina mbalimbali, kuona michezo mingi, kuangalia sinema na mchezo wa ngonjera. Bw. Wang alisema:

    "Wachezaji wengi maarufu sana wakati ule, wakiwemo Hou Baolin, Ma Lisan na Xin Fengxia waliwahi kufanya maonesho kwenye 'Ua wa Kuni', jambo ambalo liliongeza utamaduni na michezo ya jadi kwa ua huo, hata kwa mji wa Qingdao pia."


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako