Baada ya kula chakula, unaweza kutembelea jumba la jumuiya ya wazawa wa Nanjing, ambapo unaweza kutazama michezo mingi ya jadi ikiwemo ya opera za Beijing, Lu, Mao, Liu, Dagu na ngonjera, na utaburudishwa na kufahamishwa kuhusu utamaduni wa jadi wa China.
Unayosikia sasa ni opera ya kienyeji ya Liu ya Qingdao. Watu wengi wanasimama na kusikiliza opera hiyo. Mkazi wa Qingdao, shangazi Lu Xiuhua alifika kwenye jengo la jumuiya ya wazawa wa Nanjing asubuhi mapema, alisema, yeye huenda huko kuangalia kila mara inapooneshwa michezo kwenye mtaa wa Ua wa Kuni, kwani yeye anapenda sana kutazama michezo hiyo ya jadi, tena anasikia kama amerejea katika nyakati za zamani, kila anapoona meza za mraba na fomu ndefu za kizamani. Alisema:
"Nilikwenda kununua mboga, nilipoona hapa itaoneshwa opera ya Liu, niliamua kusubiri hapa, ninapenda opera za Mao, Liu na Lu toka utotoni, na ninapenda zaidi opera za Mao na Liu."
Ili kuwapokea vizuri zaidi watalii waliotoka sehemu mbalimbali za dunia, toka mwaka 2007, mtaa wa Ua wa Kuni ulifanya marekebisho. Hivi sasa mtaa huo umekuwa na sura mpya kabisa. Bw. Wang Xinan, mkurugenzi wa ofisi ya marekebisho ya sehemu ya shughuli za biashara ya mtaa wa Zhongshan, alisema, ili kuonesha vilivyo vivutio vya mtaa wa Ua wa Kuni wenye historia ya miaka 100, marekebisho ya safari hii ni kufanya ukarabati tu kuhusu majengo ya zamani, na kudumisha umaalumu wa mtaa huo. Alisema:
"Tunarejesha vyakula vyepesi vya jadi na burudani yenye umaalumu wa hapa, vilevile tutaingiza vyakula na umaalumu vinavyopendwa na watu kutoka sehemu mbalimbali za nchini na duniani. Sasa, tunajitahidi kuimarisha umaalumu wa mtaa wa Ua wa Kuni unaopendwa na watu wa kawaida, kila mtu anaweza kupata vyakula vyepesi vya wenyeji wa hapa, wewe vilevile unaweza kujiburudisha kwa vyakula hivyo vitamu."
Wakati siku kuu ya Spring, ambayo ni siku kuu muhimu zaidi ya jadi ya nchini China, ilipowadia, mtaa wa Ua wa Kuni pia ulikuwa katika wakati wenye shughuli nyingi zaidi katika mwaka, ambapo michezo yenye umaalumu wa jadi ya China ilioneshwa kwa zamu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |