• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kanasi, sehemu mpya ya michezo ya kuteleza kwenye theluji

    (GMT+08:00) 2009-03-02 17:47:29

    Kanasi iko kwenye sehemu ya milima yenye baridi kali, kwa hiyo hata katika majira ya joto, hali ya hewa ya huko siyo joto, na hewa yake ni safi sana, hivyo watalii wengi wanapenda kwenda huko katika majira ya joto. Muda wa majira ya baridi ya Kanasi ni mrefu, hali-joto ya huko inakaribia nyuzi 40 chini ya 0 kwa Celsius, theluji inadondoka kuanzia mwishoni mwa mwezi Oktoba hadi mwishoni mwa mwezi Machi mwaka unaofuata, ambapo njia zote za kuingia mlimani hufunikwa kabisa na thaluji, shughuli za utalii katika majira hayo zinasitishwa kabisa. Lakini hali hii imebadilika hivi sasa. Kundi la kwanza la watalii liliwasili Kanasi na kujifurahisha katika mazingira ya barafu na theluji ya huko.

    "Tarehe 2 mwezi Januari mwaka 2009, wapiga picha na watalii zaidi ya 500 kutoka nchini na nchi za nje walisafirishwa na magari zaidi ya 100 hadi sehemu ya Kanasi na kushiriki tamasha la upigaji picha kuhusu mandhari ya barafu na theluji ya Kanasi. Watu hao walifurahi sana kwani walikuwa wa kundi la kwanza wanaoingia sehemu hiyo katika majira ya baridi.

    Shughuli za utalii katika majira ya baridi zilifanikiwa kutokana na mitaji mingi iliyotiwa katika sehemu ya Kanasi. Katika majira ya baridi ya mwaka 2008, sehemu ya Kanasi ilinunua katapila(caterpillar) la kuondolea theluji na barafu kwa gharama ya Yuan za Renminbi milioni 3 ili kuhakikisha kupitika kwa njia inayoingia sehemu hiyo.

    Mpiga picha, Bi. Zhou Lei hapo zamani aliingia sehemu hiyo kwa kigari cha kukokotwa na farasi, safari hii alifika huko kwa kupanda basi, akieleza mawazo yake kuhusu safri hizo mbili, alisema:

    "Safari iliyopita, nilifika hapa juu kwa kutumia siku mbili, na nilishuka mlimani kwa siku mbili vilevile, nilikaa siku mbili kwenye sehemu ya juu ya mlima, kwa jumla ni siku 6. Wakati wa usiku hali-joto ilikuwa chini ya nyuzi 40, hata kipimajoto alichokuwa nacho mwenzetu wetu mmoja wa safarini kiliacha kufanya kazi kutokana na baridi kali. Njiani nilihisi kama vidole vyangu havipo tena kutokana na baridi kali, nilipata taabu nyingi. Lakini ni heri sana mwaka huu, nilifika sehemu ya juu kwa kutumia saa chache tu."


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako