• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kanasi, sehemu mpya ya michezo ya kuteleza kwenye theluji

    (GMT+08:00) 2009-03-02 17:47:29

    Katika sherehe ya ufunguzi ya upigaji picha kuhusu mandhari ya barafu na theluli iliyofanyika huko Kanasi, mkoani Xinjiang katika siku ya pili ya mwaka mpya kwa kalenda ya kilimo ya China, watazamaji walivutiwa sana na shughuli zenye umaalumu wa mila na utamaduni wa huko zinazohusu barafu na theluji zikiwemo mbio za farasi, kulenga shabaha kwa mishale na mieleka. Ingawa hali ya hewa ilikuwa baridi sana kama zaidi ya nyuzi 30 chini ya 0, lakini wapiga picha na watalii walipiga picha nyingi. Mtalii kutoka Shanghai, Bw. Ju Xingzhou ni mara ya 6 kufika Kanasi, lakini ni mara yake ya kwanza kufika huko katika majira ya baridi. Alisema:

    "Hapa panachangamsha sana, kuna vitu vingi vya asili vinavyovutia, nitakuja mara kwa mara, safari hii ninataka kutimiza lango langu, yaani nimefika hapa katika majira yote manne ya mwaka."

    Mbali na kuburudishwa na mandhari ya asili ya kupendeza sana, wapiga picha na watalii waliona mashindano ya mchezo wa kale wa kuwinda wanyama kwa kuteleza kwenye theluji, ambao watu hawawezi kuuona katika sehemu nyingine. Kanuni za mashindano hayo zinaagiza, washindani wanatakiwa kuteleza kwenye theluji kwa umbali wa kilomita 18, huku wakiwinda wanyama wa bandia waliotengenezwa kwa ngozi, mtu anayemaliza kwa haraka na kuwinda wanyama wengi zaidi, atakuwa amepata ubingwa wa mashaindano.

    Wataalamu wanasema baada ya kufanya utafiti, sehemu ya Aletai iliyoko kaskazini kabisa katika mkoa wa Xinjiang ni sehemu iliyoanza mapema zaidi mchezo wa kuteleza kwenye theluji kwa wabinadamu. Michoro ya kale iliyochorwa kwenye mawe ya milima ya huko inaonesha, kabla ya miaka elfu 10 iliyopita, wafugaji wakale wa mifugo wa sehemu ya Aletai walivumbua mbao za asili zilizotumiwa kama chombo cha kuteleza kwenye theluji, ambazo zinatumika hadi hivi sasa. Mbao hizo zinazotumika katika kuteleza kwenye theluji ni za mti wa msonobari zenye urefu wa senti-mita 180 hivi, upande wa chini wa mbao zinazoteleza kwenye theluji zinafunikwa kwa ngozi ya miguu ya farasi, na mbazo hizo zinafungwa kwenye miguu miwili kwa kamba za ngozi. Mtu anayepanda juu kwa kutumia mbao hizo, ambazo manyoya ya ngozi yanaelekea nyuma, anaweza kujituliza vizuri wakati anapopiga hatua, wakati anaposhuka, ngozi yenye manyoya laini iliyoko chini ya mbao za kuteleza kwenye thaluji inaweza kuongeza kasi ya kuteleza.


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako