• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kutembelea ngome za kale za Danba

    (GMT+08:00) 2009-03-23 16:17:04

    Wilaya ya Danba, ambayo ni sehemu yenye mandhari nzuri katika mkoa wa Sichuan, kusini magharibi mwa China. kuangalia sehemu ya magharibi ya mkoa wa Sichuan kutoka angani, mito mitano ya Dajinchuan, Xiaojinchuan, Geshizha, Donggu na Dadu inakutana kwenye wilaya ya Danba, jinsi ilivyo kama ua moja lililochanuka lenye vipande vitano. Sehemu hii ndiyo wilaya Danba inayosifiwa kuwa ni "nchi yenye ngome elfu".

    Wilaya ya Danba iko katika sehemu inayojiendesha ya kabila la Watibet ya Ganzi mkoani Sichuan, katika eneo hilo lenye zaidi ya kilomita za mraba 5,600, kuna milima mikubwa, mabonde mengi na mandhari ya asili ya kupendeza. Alipoeleza ngome zilizojengwa zaidi ya miaka elfu moja iliyopita pamoja na hadithi za kuvutia kuhusu ngome hizi, mwongoza safari ya watalii, Bw. Dan Zehng alisema,

    "Inasemekana, kabla ya miaka mingi iliyopita, sehemu ya Danba ilikumbwa na maafa ya kimaumbile mara kwa mara, mashetani wa porini nao walifanya matata, wakazi wa vilimani walikuwa na wasiwasi mkubwa, mfalme aliwaita mawaziri na mafundi kutafuta mbinu ya kuwakabili, fundi mmoja alipendekeza kujenga ngome yenye pembe nne, kimo kiasi cha mita 7, mlango mdogo wa mita 1 na dirisha lenye upana wa kiasi cha sentimita 3. Mashetani walipowavamia tena wakati wa usiku, hawakuambulia chochote. Tokea hapo, mfalme aliamuru watu wote washiriki kujenga ngome."

    Katika historia, ngome zilikuwa na uhusiano mkubwa na vita. Karibu milango ya ngome zote ilijengwa kwa urefu kati ya mita 3 hadi 7 wa kwenda juu, mbele ya mlango imewekwa ngazi, pindi maadui walipowashambulia, wanaingia ndani ya ngome, kuondoa ngazi na kufunga mlango, hivyo ni shida kwa maadui kuingia ndani ya ngome. Ngome ilikuwa na matundu ya kutupia mishale, na mishale huwatupia maadui wakiwa mbali, na kuwatupia magogo na mawe kutoka sehemu ya juu ya ngome wakiwa karibu.


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako