• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kutembelea ngome za kale za Danba

    (GMT+08:00) 2009-03-23 16:17:04

    Ngome zilikuwa minara ya kudumu nyoyoni mwa watu wa Danba, tena zimepewa uhai na hadhi. Ngome za kale ni kama binadamu, ambazo zina umaalumu wa kijinsia na majina, ngome za kike pembe zake ni mistari iliyonyooka, ambayo kila baada ya urefu fulani inapinda kwa ndani, jinsi ilivyo ni kama marinda ya wanawake, ikilinganishwa na ngome za kiume, ambazo pembe zake ni mistari iliyonyooka moja kwa moja.

    Vivutio mara kwa mara vinahusiana sana na uzuri, hali kadhalika ngome za Danba. Inasemekana, wakati enzi ya kifalme ya Xixia ilipoanguka, watu wa ukoo wa mfalme pamoja na jamaa zake waliishi mafichoni katika Danba, kwa hiyo vizazi vyake walikuwa na mwenendo bora na sura nzuri, isipokuwa hawakutazamia kwamba wangefia huko hatimaye. Mwongoza safari, Bw. Dan Zeng alisema,

    "Baadhi ya ngome zilijengwa kwa ajili ya kufanya matambiko, babu yangu alisema, chini ya kila ngome alizikwa msichana mmoja mzuri aliyefanywa kama kafara."

    Aidha, huko Danba kuna kundi la masanduku ya mawe ya kuwekea maiti ya enzi ya Neolithic, utamaduni mkubwa wenye umaalumu wa kikabila, michezo ya jadi ya kupendeza ikiwemo ngoma ya kutupa mshale kwa upinde na mbio za farasi, mila na desturi ya uchumba na ndoa ya Watibet wa Danbajiarong, pamoja na harusi na mazishi ya jadi.

    Mtu akisimama kwenye sehemu ya Danba yenye ngome nyingi za kale na kuangalia mto mkubwa Dadu, anaweza kujisikia kama yuko katika enzi ya zamani.


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako