• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maua ya cherry yachanua vizuri mjini Wuhan

    (GMT+08:00) 2009-04-13 18:32:27

    Kila mwaka kuanzia mwezi Machi hadi Aprili, wakaazi na wanafunzi wa vyuo vikuu vya mji wa Wuhan ulioko sehemu ya kati ya China wanapenda sana kwenda kutizama maua ya cherry. Miti ya maua ya cherry ya mashariki ni tofauti na miti ya maua ya cherry ya magharibi, ambayo maua yake ni ya rangi nyeupe na waridi, na yanatia fora katika majira ya Mchipuko mjini humo. Ukisimama chini ya miti ya maua ya cherry, unaweza kusikia harufu nzuri ya kipekee ya maua hayo, ukishika vipande vya maua vilivyoanguka chini, utaona ubunifu unaoletwa na maua ya cherry.

    Mtu akitaja maua ya cherry, watu wengi hufikiria Japan mara moja. Ukweli ni kwamba maua ya cherry yalikuwepo nchini China hata katika zamani za kale, ambayo yalisifiwa sana na washairi katika mashairi yaliyotungwa nao zaidi ya miaka 1,000 iliyopita.

    Kila ifikapo mwezi wa tatu, ambapo hali ya hewa ni ya majira ya Mchipuko. Upepo mwororo wa Mchipuko ukivuma kwenye milima na mashambani, vilevile unaamsha maua ya cherry yaliyolala kwa mwaka mzima. Maua yote ya miti ya cherry zaidi ya 1,000 iliyoko ndani ya chuo kikuu cha Wuhan yamechanua vizuri sana, chuo kikuu hicho kinasifiwa kuwa ni chuo kikuu kizuri zaidi kuliko vyuo vikuu vingine vya nchini China. Miti ya cherry yenye maua iliyopo kwenye chuo kikuu hicho ilipandwa kwa mistari, maua yake meupe yanaonekana kama theluji au mawingu, na kufanya chuo kikuu hicho kisicho na kelele kubadilika kuwa kama bustani yenye watu wengi. Kwenye barabara ya chuoni ya kutoka lango lenye maneno makubwa ya "Chuo Kikuu cha Wuhan cha Taifa" hadi mlima wa Lyojia, kuna halaiki ya watu wenye furaha waliofika huko kuangalia maua ya cherry. Kwenye njia inayozunguka-zunguka ya kupanda juu ya mlima, watu wanaweza kuburudishwa na maua mazuri ya miti ya cherry iliyopandwa kwenye kando mbili za njia. Roshani kubwa iliyoko kwenye bweni la wanafunzi pia ni sehemu nzuri ya kutazama maua ya cherry, mtu akisimama huko anaweza kuona miti yote ya maua ya cherry. Upepo ukivuma, maua ya cherry yanaanguka kama mvua, mtu anaweza kuona hali nyingine ya kufurahisha, hata hewa ya huko ni yenye ujoto wa Mchipuko. Watalii Chen Jing na Wang Ping kutoka mkoa wa Anhui walikuwa wakipiga picha za video bila kusita, walisema, watawaonesha wanafunzi wenzao baada ya kurudi Anhui. Walisema:

    "Sisi ni wanafunzi wa mwaka wa nne wa chuo kikuu, hivyo sasa tunapata nafasi kidogo ya kutembelea sehemu ya nje, tulisikia, maua ya cherry katika chuo kikuu cha Wuhan ni ya kupendeza sana, hivyo tumefika hapa. Maua ya cherry ya mji wa Wuhan ni mazuri kweli, vilevile yanawakilisha aina ya historia ya mji huu, ni ya utamaduni wa kipekee, chuo kikuu cha Wuhan ni chuo kikuu kinachotoa mafunzo ya elimu mbalimbali, hivyo ni chenye aina nyingi za utamaduni, hivyo kutizama maua ya cherry katika mazingira yenye utamaduni mwingi, tunasikia vizuri zaidi."

    Barabara maarufu ya maua ya cherry ya chuo kikuu cha Wuhan iko karibu na chuo cha sayansi na maktaba ya zamani, majengo hayo mawili ni majengo yanayohifadhiwa kitaifa. Mtu akisimama hapa, anaweza kuona miti ya maua ya cherry iliyoko kwenye kando mbili za barabara, maua ya cherry yanafanya majengo hayo makubwa na nadhifu kuonekana kuwa ya kupendeza zaidi, hivyo kuna msemo unaosema, "hakuna sehemu nyingine kwa watu kujiburudisha kwa maua ya cherry, ila tu chuo kikuu cha Wuhan". Ikiwa watu wanatizama maua ya cherry katika sehemu nyingine, vitu wanavyoona ni uzuri wa mandhari ya Mchipuko, lakini watu wanaotizama maua ya cherry kwenye chuo kikuu cha Wuhan, vitu wanavyoona kwanza ni kujisikia wao ni wasomi. Kusimama chini ya miti ya maua ya cherry, kutembea kwenye chuo cha kale, kuangalia vitabu vinavyouzwa kandokando ya barabara, kuangalia wachoraji wenye kuchora michoro ya mandhari, au kusikiliza msanii akipiga gita, yote hayo yanafanya watu kukumbuka nyakati waliposoma shuleni.


    1 2
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako