Miti ya maua ya cherry ilianza kupandwa kwenye chuo kikuu cha Wuhan mwaka 1939. Katika miaka mingi iliyopita, mafundi wa bustani wa chuo kikuu hicho walijitahidi kufanya utafiti kuhusu upandaji, utunzaji na uoteshaji wa mbegu za miti ya maua ya cherry, hivyo maua ya cherry yanachanua kwa muda mrefu zaidi kuliko sehemu nyingine. Chuo kikuu cha Wuhan mara kwa mara kinatoa zawadi ya mbegu za miti ya maua ya cherry zilizooteshwa na chuo kikuu hicho kwa vyuo vikuu au idara nyingine, kwa mfano, katika mwaka 1988, chuo kikuu cha Wuhan kilitoa miti maarufu 16 ya maua ya cherry, ambayo matawi yake yanainama chini kwenye chuo kikuu cha mambo ya fedha na uchumi cha Zhongnan. Mwaka 1991, kilitoa miche zaidi ya 200 karibu za aina kumi kwa bustani ya Yuyuantan ya Beijing. Hadi hivi sasa ndani ya chuo kikuu cha Wuhan kuna miti ya maua ya cherry zaidi ya 1,000, ikiwemo miti ya maua ya cherry ya kijapan, maua ya "cherry hill", maua ya miti ya cherry inayoinama matawi pamoja na maua ya cherry ya Yunnan ambayo ni ya aina nne za miti ya maua ya cherry na aina 10 za miti ya maua ya cherry iliyobadilika au ya chotara. Mafundi wa bustani wa chuo kikuu hicho wanaendelea kuchukua hatua za kiteknolojia kutunza maua ya cherry na kuotesha mbegu za aina mpya za miti ya maua ya cherry ili kufanya chuo kikuu hicho kuwa cha kupendeza zaidi.
Sehemu nyingine nzuri ya kutizama maua ya cherry katika mji wa Wuhan ni bustani ya miti ya maua ya cherry ya Donghua, ambayo iko karibu sana na chuo kikuu cha Wuhan. Sehemu hii inafanya tamasha la maua ya cherry, licha ya kutizama maua ya cherry, kuna michezo mingi ya kiutamaduni, kama vile kuweka taa zenye mishumaa kwenye maji ya mto karibu na miti ya maua ya cherry, maonesho ya picha za mandhari ya bustani tatu kubwa za maua ya cherry za dunia na maonesho ya picha kuhusu aina mbalimbali za miti ya maua ya cherry. Shughuli zinazopendwa zaidi na wavulana na wasichana wanaopendana ni kutizama maua ya cherry wakati wa usiku, taa za rangi za aina mbalimbali zimewekwa chini ya miti ya maua na kutumia sayansi ya sauti, mwangaza na umeme, miti ya maua hupendeza sana kwa kumulikwa na taa za rangi mbalimbali. Bw. Wang Chun kutoka chuo cha sayansi na teknolojia cha Wuhan, alisema,
"Hali ya hewa ni nzuri, katika siku za kawaida mimi hukaa chuoni kwa muda mrefu, nakuja kufanya matembezi, ninaona mazingira ya kijani ya majira ya Spring."
Bi. Lu Huifang, ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha wazee cha sehemu ya Hongshan ya mji wa Wuhan, yeye na wanafunzi wazee wenzake walikuwa wakipiga picha, alisema,
"Ninafurahi kila siku, na kila dakika, maua mazuri ya cherry yamepamba maisha yetu."
Katika bustani hiyo yenye hekta 10, inaota miti 500 ya maua ya cherry. Ikiwemo mkupuo wa kwanza wa miti ya maua iliyotolewa zawadi na waziri mkuu wa zamani wa Japan, Bw. Tanaka kwa waziri mkuu wa zamani wa China, Bw. Chou Enlai na mkewe, miti hiyo ilitolewa zawadi tena kwa sehemu ya Donghu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |