Kudumisha ongezeko la viwango PMI kwaonesha kufufuka hatua kwa hatua kwa uchumi wa China
Takwimu zilizotolewa kwa pamoja na Idara ya takwimu ya China na Shirikisho la usambazaji na manunuzi ya bidhaa la China hivi karibuni zimeonesha kuwa, katika mwezi Machi, moja kati ya viwango vinavyoonesha hali ya jumla ya uchumi PMI ilikuwa ni asilimia 52.4, na huu ni mwezi wa kwanza kwa kiwango hicho kufikia zaidi ya asilimia 50 baada ya kushuka chini ya asilimia 50 kwa miezi sita mfululizo. Wachambuzi wanaona kuwa, hii ni dalili ya kufufuka kwa uchumi wa China.
Kiwango cha PMI kinaonesha hali ya jumla ya mambo ya utengenezaji. Kwa kawaida kama kiwango hicho kinazidi asilimia 50, kinaonesha kustawi kwa uchumi, kinyume chake kama kiwango hicho kinashuka na kuwa chini ya asilimia 50, kinaonesha kushuka kwa uchumi. Takwimu zilizotolewa kwa pamoja na Idara ya takwimu ya China na Shirikisho la usambazaji na manunuzi ya bidhaa la China baada ya kufanya uchunguzi juu ya viwanda vya utengenezaji vya mikoa 31 kote nchini China.
Takwimu zimeonesha kuwa, ikilinganishwa na mwezi Februari, kati ya viwango mbalimbali vya PMI vilivyotolewa mwezi Machi, licha ya kiwango kinachoonesha hali ya bidhaa zinazolimbikizwa kilishuka kwa asilimia 1.0, kiwango vingine mbalimbali vyote vilidumisha ongezeko la zaidi ya asilimia 3. Kati ya viwango hivyo, viwango kuonesha hali ya uzalishaji wa bidhaa, kiasi cha orodha mpya za kuagiza bidhaa, orodha mpya za bidhaa zinazouzwa katika nchi za nje, na zile za bidhaa ambazo hazijakabidhiwa, kiasi cha manunuzi ya bidhaa, na kiasi cha bidhaa zinazoagizwa kutoka nchi za nje, vyote viliongezeka kwa zaidi ya asilimia 4.
Mtaalamu wa uchumi wa Kampuni ya Hisa ya Yinhe Bi. Zuo Xiaolei akizungumzia hali hii alisema:
"Kiwango cha PMI kinaonesha mwelekeo wa hali ya uchumi katika miezi tatu hadi sita ijayo, hivyo naona kuwa kudumisha ongezeko kwenye kiwango hicho kunaonesha kuwa, uchumi wa China utafufua kwa utulivu ndani ya miezi mitatu hadi sita ijayo."
Mkurugenzi wa Idara ya takwimu ya China Bw. Ma Jiantang pia alisema, kuinuka kwa kiwango cha PMI na mabadiliko aliyoona alipofanya uchunguzi na utafiti kwenye sehemu mbalimbali nchini China kumeonesha kuwa, hatua mbalimbali za serikali katika kupanua mahitaji kwenye soko la ndani, kuhimiza ongezeko la uchumi, kurekebisha miundo ya bidhaa, kukuza mageuzi na kuboresha maisha ya wananchi zimepata ufanisi mzuri, pia kumeonesha kuwa uchumi wa China utafufuka hatua kwa hatua.
Wakati huo huo, kampuni mbalimbali za hisa za China hivi karibuni pia zimetoa makadirio kuwa, mwelekeo wa hali ya jumla ya uchumi wa China utakuwa mzuri zaidi. Mkurugenzi wa utafiti wa Mfuko wa Yinhua Bw. Jinbin alisemaļ¼
"Takwimu zilizotolewa katika miezi kadhaa iliyopita zimeonesha mwelekeo mzuri, na utakuwa mzuri zaidi katika siku za mbele."
Lakini mtaalamu wa uchumi wa Kampuni ya hisa ya Yinhe Bi. Zuo Xiaolei alisema, kati ya viwango mbalimbali vya PMI vya mwezi Machi, kiwango kinachoonesha orodha mpya za bidhaa zinazouzwa katika nchi za nje kilikuwa ni asilimia 47.5, ingawa kiasi hicho kiliongezeka kwa asilimia 4.1 kuliko mwezi Februari, lakini bado kiko kwenye kiwango cha chini, hali ambayo inaonesha kuwa hali ya uuzaji wa bidhaa katika nchi za nje bado si nzuri. Alisema:
"Sera mbalimbali za China zikiwemo kurudisha ushuru kwa bidhaa zinazouzwa katika nchi za nje zinaweza tu kutoa misaada kwa kiasi. Kwani uuzaji wa bidhaa katika nchi za nje unahusiana sana na soko la kimataifa, na hali hii haitabadilika kabisa bila ya kuboreshwa kwa hali ya soko la kimataifa. Ingawa hali ya uuzaji wa bidhaa katika nchi za nje imeboreshwa kwa kiasi, lakini nadhani kuwa haipaswi kutegemea serikali kutoa sera mbalimbali zenye misaada kuleta mabadiliko makubwa zaidi."
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |