• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maua mazuri na vyakula vya jadi vyaongeza sifa za Qujing

    (GMT+08:00) 2009-05-04 17:04:37

    Mto Lulu ni mto mkubwa kabisa kwenye sehemu ya kusini ya China, mto huu unapita kwenye mikoa mingi na umevumbua historia na utamaduni unaong'ara wa sehemu ya kusini pamoja na ustawi wa delta ya mto Lulu. Mji wa Qujing ulioko sehemu ya kusini magharibi ya mkoa wa Yunnan ni chanzo cha mto Lulu, hivyo unaitwa kuwa ni "mji wa kwanza wa Mto Lulu".

    Qujing iko kwenye sehemu ya kati ya uwanda wa juu wa Yungui, inapakana na mikoa ya Guizhou na Guangxi kwa upande wa mashariki, na kupakana na Kunming, mji mkuu wa mkoa wa Yunnan kwa upande wa magharibi, kusini mwake kuna mlima Lianwen, mto Mwekundu, na sehemu yake ya kaskazini ipo Shaotong na Bijie ya mkoa wa Guizhou, Qujing ni njia muhimu ya kuunganisha mkoa wa Yunnan na sehemu ya bara ya China, kuna msemo usemao, Qujing ni "kufuli na ufunguo wa Yunnan na Guizhou", "mlango wa kuingia Yunnan".

    Mji wa Qujing wenye eneo la zaidi ya kilomita za mraba elfu 28, ni mji mkubwa unaochukua nafasi ya pili ukifuata mji wa Kunming, vilevile ni mji muhimu wa viwanda na kilimo wa Yunnan. Msafiri mashuhuri wa enzi ya Ming, Xu Xiake aliwahi kutembelea huko, aliandika makala ikisema chanzo cha mto Lulu kiko kwenye mji wa Qujing. Kwa kuwa Qujing ni chanzo cha mto Lulu, hivyo kila mwaka kuna idadi kubwa ya watalii wanaoitembelea. Mtalii kutoka Hongkong, Wang Jiafu alisema,

    "Kivutio cha chanzo cha mto Lulu ni sehemu ya lazima kutembelea mkoani Yunnan, ili kushuhudia chanzo cha mto. Hapa ni bustani ya misitu ya kitaifa, mandhari yake ni ya kuvutia sana, na ni mahali pazuri kwa mapumziko."

    Luoping na Shizong zilizoko kusini mwa mji wa Qujing pia ni sehemu zenye vivutio. Maua ya kupendeza huchanua vizuri sana katika majira ya Mchipuko. Katika mwezi Februari na Machi maua ya rangi ya manjano ya rape yanatandaa sehemu nzima ya Luoping, mandhari nzuri yanavutia watalii na wapiga picha wa sehemu mbalimbali. Naibu mkuu wa wilaya ya Luoping, Zhang Xikang alisema,

    "Hivi sasa wilaya ya Luoping imepanda zao la rape kwa zaidi ya hekta elfu 40, zao hilo limeleta nafasi nzuri kwa maendeleo ya utalii ya wilaya yetu. Zao hilo peke yake limeongeza pato la wastani wa Yuan 300 kwa kila mkulima kati ya wakulima laki 5.2 wa wilaya yetu."

    Ikilinganishwa na rape ya Luoping, miti mikubwa ya maua ya azalea kwenye mlima Junzi wa sehemu ya Shizong pia ni kivutio kikubwa. "Azalea ya miaka elfu moja" ni aina maalumu ya maua ya huko, mtaalamu amethibitisha kuwa mti ulioota miaka mingi zaidi ni ule wa zaidi ya miaka 1,600 iliyopita. Miti ya aina hiyo inachanua maua katika mwezi Februari hadi Machi kwa siku 40 hivi, rangi ya maua hayo ni nyekundu. Maua yanapochanua kwa wingi yanaburudisha watu sana, umbo la ua la azalea ni zuri sana, sehemu yenye maua hayo ni moja kati ya sehemu zenye mandhari nzuri kwenye mlima Junzi. Bi. Zhang Changqin profesa wa taasisi ya mimea ya mji wa Kunming, anatembelea huko mara kwa mara, kila mwaka maua ya azalea yanapochanua, yeye hufika huko.


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako