Qujing imefanya mara 4 shughuli za "wiki ya utamaduni wa vyakula vitamu vya chanzo cha mto Lulu toka mwaka 2004. Hivi sasa utalii wa chakula kitamu umeendelezwa vizuri Qujing.
Sekta ya utalii ya Qujing imepata maendeleo mazuri. Mwaka 2008 ilipokea watalii milioni 5.7 wa nchini na wa nchi za nje, pato la sekta hiyo lilifikia Yuan bilioni 2.76. Mkurugenzi wa idara ya utalii ya Qujing, Zhai Qingyun alisema,
"Sasa tumeweka mpango wa maendeleo wa kipindi cha pili kuhusu uimarishaji wa afya na mapumziko. Hapo baadaye, hadhi ya Qujing itainuka zaidi katika mkoa wa Yunnan, na kuwa kivutio kipya na kikubwa cha utalii."
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |