• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mradi wa maonesho ya kimataifa ya Shanghai

    (GMT+08:00) 2009-05-18 16:08:27

    Watu wengi sasa wanajua kuwa maonesho ya kimataifa ya mwaka 2010 yatafanyika Shanghai,China. Tangu maonesho ya kimataifa ambayo yanafanyika kila mwaka yaanzishwe mwaka 1851, mpaka sasa yamefanyika mara 124 katika nchi 30. Maonesho hayo yanaonesha maendeleo ya kisasa katika sekta za sayansi, teknolojia, utamaduni, sanaa, majengo na katika maisha ya watu na kuhimiza duru jipya la kujifunza, ushindani na maendeleo. Maonesho ya kimataifa ya mwaka 2010 yanaandaliwa na China, na yatafanyika katika mji wa Shanghai, yakiwa na kauli mbiu ya "miji bora, maisha bora".

    Majengo ya maonesho ya kimataifa ya Shanghai yako kwenye sehemu ya kusini ya mji wa Shanghai, eneo la majengo hayo ni kilomita za mraba 5.28, zikiwemo kilomita za mraba 3.28 za maonesho na kilomita 2 za kijiji cha maonesho ya kimataifa na zana za miundo mbinu. Mfanyakazi wa ofisi ya uenezi ya idara ya maonesho ya kimataifa ya Shanghai, Bi. Diao Feicui alisema,

    "Eneo la kilomita za mraba 3.28 za maonesho limegawanyika katika sehemu 5 ndogo za A, B, C, D, E, maoensho ya nchi za Asia yako kwenye sehemu ya A. Sehemu ya B ambayo ni sehemu ya kati na ni majengo ya kudumu, yakiwemo Jumba la China, kituo cha michezo, Kituo cha maonesho ya kimataifa, Jumba la tafsiri ya kauli mbiu, na majumba ya maonesho ya nchi za kanda ya Oceania na maonesho ya mashirika ya kimataifa. Sehemu ya C ni majumba ya maonesho ya nchi za Ulaya, Afrika na bara la Amerika. Maonesho ya nchi zote pamoja na ya mashirika ya kimataifa yako kwenye upande wa mashariki ya mto Huang-pu, upande wa magharibi wa mto Huang-pu ni sehemu ya D, ambayo ni ya majumba ya maoensho ya kampuni na viwanda. Sehemu ya E ni kuhusu uzoefu bora wa miji, ambapo utaonekana uvumbuzi wa Maonesho ya kimataifa ya Shanghai na kuwa kivutio kimoja cha maonesho hayo, ili kuendana na kauli mbiu ya maonesho hayo, tumechagua mifano bora ya ujenzi wa miji ya duniani, ili ioneshwe kwenye maonesho ya Shanghai."

    Umaalumu wa maoensho ya kimataifa ya Shanghai ni "mstari wa kati na kumbi nne", ambayo ni mstari wa kati wa maoensho ya kimataifa, ukumbi kuhusu kauli mbiu, ukumbi wa China, kituo cha maoensho ya kimataifa na kituo cha michezo.


    1 2 3 4
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako