• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mradi wa maonesho ya kimataifa ya Shanghai

    (GMT+08:00) 2009-05-18 16:08:27

    Naibu mkurugenzi wa idara ya maonesho ya kimataifa, Bw. Huang Jianzhi alitufahamisha kuhusu jengo lililo kubwa kabisa kwenye eneo la maonesho. Alisema:

    "Ujenzi wake unatumia teknolojia ya bonde la mwanga wa jua, sehemu ya juu ya jengo hilo ni kubwa na sehemu yake ya chini ni ndogo, lengo lake ni kuleta mwanga wa jua hadi kwenye sehemu ya chini ya ardhi."

    Kati ya majengo ya maonesho, jengo la kituo cha michezo linaonekana kuwa na harufu nzito ya usanii, mtoa maelezo wa maonesho hayo, dada Zhang Xi alisema:

    "Umbo la kituo cha michezo ni kama sahani, ambalo linapendeza sana, sifa yake kubwa ni kuweza kurekebisha idadi ya viti vyake kwa kufuata idadi ya watazamaji. Kwa wingi mkubwa jengo hilo linaweza kuwachukua watu elfu 18, na kwa uchache kabisa linaweza kuchukua watu elfu 4."

    Ili kusisitiza kauli mbiu ya maoensho ya kimataifa ya Shanghai, imejenga mahsusi Jumba la tafsiri ya kauli mbiu ya maonesho hayo, ili kufanya utafiti juu ya uhusiano kati ya miji, watu, uhai na sayari katika siku za baadaye. Maonesho ya jumba hilo yanagawanyika katika sehemu mbili, zote zinazingatia wazo la kubana matumizi ya nishati na hifadhi ya mazingira ya asili.Bi. Zhang alisema:

    "Kuna sehemu iliyoinama kwenye paa la jumba hilo, ambayo inatumika kukusanya maji ya mvua, maji hayo yanatumiwa kuimwagilia mimea iliyoko kwenye eneo la maonesho."


    1 2 3 4
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako