• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mji wa Suzhou wenye mtindo wa kale na wa kisasa pamoja

    (GMT+08:00) 2009-05-25 21:14:53

    Maonesho ya kimataifa ya Shanghai ya mwaka 2010 yatafanyika baada ya muda usiofikia mwaka mmoja kuanzia sasa, kama ukitaka kutembelea Shanghai wakati wa maonesho ya kimataifa, ni vizuri ungepanga safari yako vyema, kwani kuna vivutio vingi kwenye sehemu ya pembezoni mwa mji wa Shanghai. Kuna msemo mmoja wa kichina usemao "mbinguni kuna pepo, duniani kuna Suzhou na Hangzhou". Katika kipindi hiki cha leo tutawafahamisha kuhusu mji wa Suzhou.

    Mji wa Suzhou mkoani Jiangsu uko kwenye sehemu ya kati ya delta ya Mto Changjiang, kwa upande wa mashariki unakaribiana na mji wa Shanghai, kwa upande wa kusini unapakana na mkoa wa Zhejiang, upande wa magharibi kuna Ziwa Taihu, na upande wa kaskazini kuna Mto Changjiang. Ili kuhifadhi sura ya mji wa kale wa Suzhou, katika mpango wa maendeleo ya mji, mji huu umegawanyika katika sehemu mbili za mji wa kale na eneo jipya la viwanda. Sasa sura maalumu ya mji wa kale wa Suzhou imedumishwa, ambayo kuna mtaa unaokwenda sambamba na mto, kuna madaraja madogo, nyumba zenye mtindo wa zamani zenye kuta za rangi nyeupe zilizoezekwa kwa vigae vya rangi ya kijivu nzito iliyokolea, bustani maarufu zilizojengwa zamani za kale pamoja na vivutio vingi vinavyojulikana sana kutoka zamani.

    Mtaa maarufu wa Shantang unasifiwa kuwa ni "mtaa maarufu wa kwanza wa mjini Suzhou", majengo yaliyoko kwenye mtaa huu ni mazuri, yakiwa ni pamoja na nyumba za makazi na maduka, ambazo zimepangwa vizuri na kuwavutia watu. Hususan katika wakati wa usiku, taa nyingi za rangi nyekundu za jadi za kichina zinawashwa, sauti ya opera ya Pingtan ya Suzhou inasikika kwa mbali ikichanganyika na sauti ya mtiririko wa maji ya mto. Mtalii kutoka Singapore, Bw. Huang Enling alisema,

    "Hapa ni mahali pazuri sana, tunaweza kuhisi utamu wa mji wa kale."

    Baada ya kutembelea Mtaa wa Shantang, kama bado una shauku, bora uende kujiburudisha kwa chai iliyopikwa kwa maji ya Ziwa Taihu, na kusikiliza opera ya Pingtan ya Suzhou, ambayo sauti yake ni nyororo na iliyoimbwa taratibu.

    Kama ilivyo kwa mgeni kwenda kusikiliza opera ya kibeijing baada ya kufika mjini Beijing, mgeni asipokwenda kusikiliza opera ya Pingtan baada ya kufika Suzhou, utamu wa safari yake utapungua sana. Lakini ikiwa utaona Suzhou ni mji wenye mtindo wa kale na mtindo wa taratibu sana wa maisha, basi utakuwa umekosea.


    1 2
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako