• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mji wa Suzhou wenye mtindo wa kale na wa kisasa pamoja

    (GMT+08:00) 2009-05-25 21:14:53

    Muziki huu unaweza kuchukuliwa kuwa ni alama ya Uwanja wa Shidai Yuanrong wa Suzhou. Kivutio kikubwa kwenye uwanja huu ni njia moja ndefu yenye taa nyingi inayojulikana kama "skrini kubwa ya kwanza la duniani", ambayo ni inasifiwa kama ni pazia la mbingu. Njia hii ina urefu wa mita 500 na upana wa mita 32, lakini ina taa zaidi ya milioni 20 za aina ya LED, ambazo zimegharimu Yuan za Renminbi karibu milioni 100. Huku kumekuwa sababu moja ya kwenda kwenye Uwanja wa Shidai Yuanrong kwa watalii wengi. Mmarekani Bw. Rico Harrison alitumwa Kwenda Suzhou kikazi, pia alikwenda kushuhudia "pazia la mbingu". Bw. Rico Harrison alisema,

    "Hata mimi siwezi kuamini, skrini hiyo kubwa imenipa kumbukumbu nyingi. Ninapenda sana "pazia hilo kubwa la mbingu", picha zinazooneshwa zinaendeshwa kwa kompyuta na zinahusu hali halisi ya maisha."

    Mtalii mwingine Bw. Shawn James alisema, kabla ya hapo aliwahi kuona skrini kubwa ya LED, lakini hiyo ya Suzhou ni kubwa na ndefu ya kushangaza. Alisema,

    "Mambo yanayooneshwa kwenye skrini hiyo ni mengi zaidi, na yanahusu mambo yanayoonesha umaalumu wa Suzhou."

    Mpendwa msikilizaji, kama umewahi kufika kwenye jumba la michezo la taifa la China na kuingia kwenye "Kiota" kikubwa kilichojengwa kwa chuma cha pua, basi baada ya kufika Suzhou lazima uende kutembelea kituo cha sayansi, teknolojia, utamaduni na sanaa cha Suzhou, ambacho kinaitwa "Kiota" kidogo. Hiki ni jengo lenye umbo la mwezi mchanga, ambalo pembe zake mbili zinaelekea kwenye upande wa Ziwa Jinjihu. Ukitazama kutoka angani, jengo hilo linaonekana kama Chaza wa majini aliyekumbatia lulu.

    Jengo hilo ni sawa na "Kiota" cha Beijing, ambalo lilisanifiwa na Bw. Paul Andrew, bingwa msanifu wa Ufaransa, muundo wake ni wa chuma na chuma cha pua, jengo hilo lina mitindo miwili ya kisasa na kizamani. Mwelezaji wa kituo hicho, Bi. Shen Jingjing alisema,

    "Vitu kadhaa vya kimsingi vya bustani za Suzhou vimetumika kwenye ujenzi wa ua wa ndani wa jengo. Ukitazama kutoka karibu, sehemu ya nje ya ukuta wa madini wa skrini inaonekana kama nyuzi za mdudu wa hariri zilizokuzwa, kutazama kutoka mbali jengo hilo kama limefunikwa na kitambaa cha hariri, hii inamaanisha kuwa Suzhou ni maskani ya kitambaa cha hariri. Ndani ya ukuta wa skrini, kuna taa za LED zaidi ya elfu 20, ambazo zinaonesha rangi mbalimbali kutokana na hali tofauti ya voti za umeme. Ukuta wa skrini umetengenezwa kwa vitu vingi vyenye maumbo ya pembe 6 kwa kuiga sanaa ya utengenezaji wa madirisha ya bustani za ki-suzhou."

    Licha ya kuwa na umbo zuri, kituo cha sayansi, teknolojia, utamaduni na sanaa cha Suzhou kina uwezo mkubwa. Kituo hicho kina ukumbi wa michezo wenye zana za kisasa na viti 1,200, ukumbi wa chakula unaoweza kuchukua watu 500, ukumbi mkubwa wa sinema wa aina ya IMAX na vyumba 7 vya sinema, ukumbi wa sayansi na teknolojia, pamoja na kituo cha shughuli za biashara chenye mita za mraba 23,000.

    Mji wa kale wa Suzhou pia una jengo moja jipya lenye mtindo wa kizamani na umaalumu wa Suzhou kama ilivyo kituo cha sayansi, teknolojia, utamaduni na sanaa cha Suzhou, jengo hilo ni jumba jipya la makumbusho la Suzhou, ambalo lilisanifiwa na bingwa msanifu Bei Yuming kabla ya kuacha kabisa kazi za usanifu, jengo hilo linachukuliwa na bingwa Bei Yuming kama ni "binti mdogo anayependwa zaidi". Usanifu wa jengo hilo umetumia mtindo wa bustani wa kizamani za Suzhou, ambapo mianzi na miti imepandwa ili kuongeza uzuri wa jengo, nalo linawavutia sana watu kwa usanifu wake murua na mpangilio mzuri wa ndani ya jumba hilo la maonesho.


    1 2
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako