• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nakupeleka kuangalia maonesho ya kimataifa ya Shanghai

    (GMT+08:00) 2009-06-15 16:53:50

    Maonesho ya kimataifa ya Shanghai yatafunguliwa mwezi Mei mwaka ujao, leo tutawatembeza kwenye maonesho hayo yatakayofunguliwa siku za usoni.

    Wimbo mliosikia ni wimbo wa maonesho ya kimataifa unaoitwa "Mji Wangu". Kwenye eneo la maonesho ya kimataifa, licha ya majengo ya kudumu, pia kuna majengo mengi ya muda, ambayo mengi ni majumba ya maonesho yaliyojengwa na nchi za nje na za kupangisha. Kwa kufuata desturi ya maonesho ya kimataifa, majengo hayo ya muda yatabomolewa baada ya maonesho kumalizika. Hii ingawa inasikitisha watu, lakini baada ya maonesho ya nusu mwaka uvumbuzi wao na wazo linalooneshwa vitabaki mioyoni mwa watu. Hivi sasa watu hawawezi kufahamu vitu vitakavyooneshwa kwenye majumba ya nchi mbalimbali, lakini usanifu wa majumba ya maonesho unashangaza watu.

    Jumba la Uingereza

    Hebu, twende kuangalia Jumba la Uingereza. Bi. Carma Elliot wa jumba hilo la Uingereza katika Maonesho ya kimataifa ya Shanghai ya mwaka 2010 alisema, jumba hilo la maoensho ni zawadi ya watu wa Uingereza kwa watu wa China. Lina kimo cha ghorofa 6, eneo lake ni mita za mraba 6,000, nje kuna mikono elfu 70 iliyotengenezwa kwa plexiglass, na urefu wa kila mkono ni kiasi cha mita 8, mikono hiyo inaweza kutetereka kidogo chini ya upepo mwororo, watu wanahisi kuwa hili ni jumba lenye uhai. Wakati giza linapoingia, jumba hili linaonekana ni la ajabu sana. Bi. Carma Elliot alisema,

    "Mikono elfu 70 ya jumba letu inatoa mwanga mdogo wakati wa usiku, inaonekana kama ni wadudu wanaotoa mwanga. Jumba letu liko kwenye kando ya mto, hivyo jumba letu ni la kipekee na la kuvutia zaidi. Hata unaweza kuuona ukiwa ng'ambo ya Mto Huangpu.

    Bi. Carma Elliot alieleza, mikono hiyo ya Jumba la Uingereza ni kama karatasi ya kufungia zawadi hiyo, kuingia ndani ya jumba hilo ni kama kuondoa karatasi hii ya kufungia zawadi, utaweza kuona zawadi yenyewe ni kitu gani. Bi. Carma Elliot anatarajia kuwa mshangao huo utatunzwa hadi siku ya ufunguzi wa maonesho ya kimataifa, kwa hiyo hakueleza zawadi hiyo ni kitu gani hasa. Kauli mbiu ya Jumba la Uingereza ni "jumba la uvumbuzi", anatarajia kuwa watazamaji wote wanaofika kwenye Jumba la Uingereza wahisi kama wamefika katika bustani isiyo na kelele ingawa wako kwenye mji wenye pilikapilika na kelele nyingi. Mbali na hayo, huenda habari nyingine itawafurahisha sana mashabiki wa soka, Bi. Carma Elliot alisema, Uingereza inatarajia kuwaalika watu mashuhuri akiwemo David Beckham, waje Shanghai kuwafahamisha watu kuhusu utamaduni wa Uingereza.

    Jumba la Ufaransa

    Nchi nyingi zinatarajia kuwafahamisha watu kuhusu utamaduni wao. Ufaransa pia ni moja kati ya nchi hizo, naibu mkurugenzi wa maonesho ya kimataifa ya Shanghai, Bw. Huang Jianzhi alisema, Jumba la Ufaransa litaonesha "mji wenye hisia". Kwa sababu Jumba la Ufaransa linajengwa kwenye maji, maji yanaweza kutumiwa mara nyingi, yanaweza kupunguza joto katika majira ya joto, kwenye paa la jumba hilo kuna bustani yenye mtindo wa kifaransa, watu wanatembelea huko kuanzia sehemu ya juu kwenda chini. Bw. Huang alisema:

    "Viongozi wa maonesho wanasema, mji unatakiwa kujulikana kwa kila mwanamji, lakini je mtu anaufahamu mji namna gani? Mtu anafahamu mji kwa hisia zake za kuona, kusikia, kunusa, kuonja na kugusa. Wanataka kukufahamisha kuhusu vitu bora vya utamaduni wa Ufaransa kwa kutumia nafasi hiyo. Kitu hasa unachohisi utajua mwenyewe baada ya kutembelea Jumba la Ufaransa. Mwandishi wetu wa habari alikwenda kuwahoji kuhusu hayo, walimwambia ni manukato ya Ufaransa."


    1 2
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako