• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nakupeleka kuangalia maonesho ya kimataifa ya Shanghai

    (GMT+08:00) 2009-06-15 16:53:50

    Mbali na kuhisi utamaduni na kushuhudia sayansi na teknolojia na kujionea wazo la maisha, kitu muhimu zaidi kufika katika maoensho ya kimataifa ya Shanghai ni kupata furaha. Jumba la Uholanzi litakupa furaha kubwa, jina la jumba hilo linaitwa "mtaa wa furaha". Kivutio kikubwa ni taa zinazowaka na kuzimika kwa kufuata utaratibu uliowekwa. Hili ni jengo ambalo mtaa uliojengwa ndani yake unazunguka na kuelekea juu, baada ya kufika kwenye sehemu ya juu mtu anaweza kuona mitaa na majengo ya baadaye ya Uholanzi. Kiongozi wa ofisi ya mambo ya maonesho ya kimataifa ya Uholanzi, Bw. Wei Weili alisema,

    "Uholanzi imekusanya baadhi ya wasanifu wanaofanya uvumbuzi kwa kufuata kauli mbiu ya "miji bora, maisha bora", "miji ya furaha" na mitaa ya furaha. Mtaa wa Uholanzi unaonesha shughuli za biashara, vilevile unafanya watu wahisi kuwa wanaweza kuishi vizuri zaidi kwenye mtaa huu wa furaha."

    Jumba la Korea ya Kusini

    Mbali na majumba hayo matatu, majumba ya Korea ya kusini, Japan, Italia na Canada yana mipango yake, na baadhi yake yameanza kazi za ujenzi, inaaminika kuwa wakati Maonesho ya kimataifa ya Shanghai yatakapofunguliwa tarehe 1, Mei, watazamaji wataweza kuona maonesho yaliyokusanya busara za watu kutoka nchi mbalimbali.

    Lengo la Maonesho ya kimataifa ya Shanghai ni kuvutia watazamaji milioni 70, wakati ule hali ya kupanga foleni kwenye majumba mengi ya maonesho itaonekana, hata hivyo usiwe na wasiwasi, licha kuweko maonesho mengi murua kwenye majumba ya maonesho, huko pia utaweza kuona maonesho ya michezo ya kiutamaduni ya nchi mbalimbali. Naibu mkurugenzi wa idara ya maonesho ya kimataifa Bw. Hu Jinjun alisema, viwanja vya maonesho ya michezo ya kiutamaduni ya Maonesho ya kimataifa ya Shanghai vitakuwa vikubwa zaidi katika historia, tunatarajia kutoa mazingira mazuri kwa nchi washiriki wa maoensho, na kuziwezesha kujionesha kwa walimwengu kutokana na michezo yao ya kiutamaduni. Alisema:

    "Kuna majukwaa rasmi ya michezo, vilevile kuna majukwaa ya michezo ya uwanjani, ambayo yataoneshwa maonesho ya michezo ya sanaa zaidi ya 100 kwa siku."

    Jumba la Japan

    Maonesho murua ya michezo ya sanaa ni pamoja na shughuli kwenye ufunguzi, shughuli za uzinduzi wa maonesho, shughuli za siku ya majumba ya nchi mbalimbali, na shughuli za kufungua na kufunga maonesho ya kimataifa. Vilevile yataoneshwa maonesho ya taa na maonesho ya zana kubwakubwa wakati wa kufunga mlango wa maonesho kila usiku, na kutakuwa na maonesho ya fashifashi katika wikiendi na siku maalumu.

    Aidha nchi washiriki wa maonesho zitaweza kuonesha mali za urithi wa utamaduni usioonekana kwa kupitia maonesho ya michezo ya kiutamaduni, shughuli za uwanjani na ukusanyaji wa usanifu. Katika muda wa miezi 6 wa Maonesho ya kimataifa ya Shanghai, shughuli zenye kauli mbiu maalumu zitafanyika kwa kufuata mpangilio wa Ulaya, Afrika, Amerika, Oceania, Asia na China.


    1 2
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako