• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nyumba za wakazi zenye umaalum katika sehemu ya kusini mwa China

    (GMT+08:00) 2009-11-02 20:24:01

    Sehemu ya Chaoshan, iliyoko kwenye pwani ya kusini mashariki mwa China, iko kwenye sehemu ya mpaka kati ya mkoa wa Guangdong na mkoa wa Fujian. Sehemu hiyo inapakana na milima kwa pande tatu, na kwenye upande mmoja kuna bahari. Toka zamani za kale, wakazi wengi wa sehemu hiyo walikwenda kujiendeleza katika nchi za nje, baada ya kujiendeleza walitoa misaada mingi kwa ajili ya maendeleo ya maskani yao. Sasa tunawafahamisha kuhusu nyumba ya zamani ya Bw Chen Cihong, ambaye ni mchina mashuhuri anayeishi katika nchi ya nje, na umaalumu wa majengo ya huko pamoja na historia ya wafanyabiashara wa sehemu ya Chaoshan.

    Nyumba ya zamani ya Bw Chen Cihong yako kwenye sehemu ya Chenghai ya mji wa Shantou, mkoani Guangdong. Hii ni sehemu yenye mandhari nzuri ya majengo maalumu ya wachina wanaoishi katika nchi za nje. Nyumba ya Bw Chen Cihong licha ya kuwa na umaalumu wa jadi ya Chaoshan, pia ina mtindo wa majengo ya nchi za nje, hivyo inasifiwa kuwa ni "Bustani yenye mandhari kubwa na nzuri kwenye sehemu ya kusini ya China" na "Nyumba ya kwanza ya kusini mwa Lingnan", majengo ya nyumba hiyo yanavutia watalii zaidi ya milioni moja wa nchini na kutoka nchi za nje.

    Mwenye nyumba hiyo hayati Chen Cihong, hapo awali aliendesha shughuli zake za biashara nchini Thailand. Alirejea kwao kujenga nyumba alipokuwa na umri wa miaka zaidi ya 50 akiwa na wazo la kuuletea fahari na heshima ukoo wake, na kuomba ajaliwe kuwa na watoto na wajukuu wengi. Meneja wa sehemu hiyo yenye mandhari nzuri ya utalii Bw Tang Xuewei alisema, kitendo chake hicho kilionesha nguvu ya kiuchumi ya familia za wachina wa Chaoshan wanaoishi katika nchi za nje. Alisema

    "Mwanzoni walifanya biashara ya mchele, halafu baadaye walianza kuendesha shughuli za benki na bima. Hapo baadaye walikuwa na kundi la meli za kufanya shughuli za uchukuzi baharini, wao walikuwa hodari sana. Wakati ule alichukua nafasi ya kwanza nchini Thailand alipofanya biashara ya mchele, aliunda matawi ya kampuni yake Hong Kong, miji ya Tianjin, Shanghai na Guangzhou, Singapore, Taiwan na Malaysia. Inasemekana kuwa alijenga makazi yake kwa kutumia kiasi cha sarafu kubwa za fedha milioni 4, ambazo zilikuwa ni fedha nyingi sana kwa wakati ule."


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako