• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maisha mapya ya wakazi wa kijiji cha Xiagei cha kabila la Watibet

    (GMT+08:00) 2009-11-12 14:57:00

    Katika mji wa Shangri-la ambao ni mji mkuu wa wilaya inayojiendesha ya kabila la Watibet ya Diqing mkoani Yunnan, kuna kijiji kimoja maarufu. Ingawa kijiji hicho kiitwacho kijiji cha Xiagei kina familia 22 za wakulima tu, lakini kilisifiwa kama kijiji cha kwanza katika sehemu ya Shangri-la kutokana na ustawi wa utalii wa utamaduni wa kitibet.

    Kijiji cha Xiagei kina umbali wa kilomita 13 kaskazini mashariki mwa mji wa Shangri-la. Maana ya neno la Xiagei katika lugha ya kitibet ni "Kijiji juu ya Mawe ya Fedha", kwa kuwa katika kijiji hicho, kuna chemchemi ya maji moto inayozingirwa na mawe yenye rangi ya kifedha.

    Kijiji cha Xiagei kiko ndani ya milima yenye misitu ya kiasili, na kupitiwa mto mmoja mzuri. Wakazi wote wa kijiji hicho ni wa kabila la Watibet, na wanadumisha vizuri mila na desturi za kabila hilo. Katika kijiji cha Xaigei, majengo ya aina mbalimbali ya kidini yanaonekana hapa na pale. Mambo hayo ndiyo vivutio kwa watalii kutoka sehemu mbalimbali.

    Bw. Kelzang Gyatso anashughulikia kuwapokea watalii katika kijiji cha Xiagei. Alisema watalii wanakwenda kijiji hicho kutokana na kuvutiwa na mila na desturi ya kitibet na vitu vya kisanii vinavyotengenezwa kwa mikono. Alisema,

    "Kijiji chetu ni cha kabila la watibet. Watalii wanaweza kuelewa mila na desturi, ufundi na sanaa, na utamaduni wa kidini wa kabila letu. Tuna desturi ya kutengeneza wenyewe vitu vinavyotumiwa katika maisha ya kawaida na mambo ya kidini. Vitu hivyo ni pamoja na vifaa vya ubao, picha za Thangka, sanamu za pembe za nzao wenye manyoya marefu, ubani wa kitibet na vyombo vya kitibet vilivyotengenezwa kwa fedha."


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako