• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maisha mapya ya wakazi wa kijiji cha Xiagei cha kabila la Watibet

    (GMT+08:00) 2009-11-12 14:57:00

    Bw. Wangdu mwenye umri wa miaka 45 ni fundi wa kutengeneza ubani wa kitibet. Ubani huo unategenezwa kwa dawa za kitibet, na unapendwa sana na watu kutokana na kuwa na harufu nzuri na thamani ya matibabu. Miaka mitatu iliyopita, Bw. Wangdu alijifunza ufundi wa kutengeneza ubani wa kitibet, na kuanzisha duka la kuuuza. Baada ya kumaliza kazi za kilimo, anatengeneza ubani huo nyumbani. Alisema,

    "Zamani tunapata mapato kutokana na kazi za kilimo tu, hivi sasa tunaweza kupata zaidi ya yuan elfu moja kwa kuuza ubani tu. Maisha yetu yameboreshwa, na tumenunua vifaa na mitambo mingi ya umme inayotumiwa nyumbani."

    Katika miaka ya hivi karibuni, shughuli za utalii mjini Shangri-la zimeendelezwa siku hadi siku. Ili kuhifadhi mazingira ya asili na kupata maendeleo endelevu, serikali katika mji huo inatoa ruzuku kwa wakulima kutoka mapato ya utalii. Wakati inapowasaidia katika uzalishaji wa kilimo, serikali pia inawahamasisha wakulima kujishughulisha sanaa za kijadi, na kujiongezea mapato kwa kuzalisha na kuuza mazao yenye umaalumu ya kilimo na vitu vya kisanaa. Naibu meneja mkuu wa bustani ya kitaifa ya Pudacuo ya wilaya ya Shangri-la Bw. Ding Wengdong alisema,

    "Tunawasaidia wakulima kufanya vizuri kazi za kilimo. Tunawasaidia kuuza mazao ya kilimo, kuwafundisha elimu za kimsingi, na kuwahamasisha kujishughulisha na ufugaji, ili kuendeleza uchumi wa mzunguko. Wakati huo huo, pia tunaongeza mitaji kwa miradi ya utamduni. Tumeanzisha vikundi vya maonesho ya nyimbo na ngoma ya wakulima, kuwashirikisha wakulima katika uzalishaji wa vitu vya kisanaa, ili kuwatajirisha. Kwa mfano tumejenga kijiji cha Xiagei kuwa ni kijiji cha kikabila chenye mazingira mazuri ya asili na utamaduni mkubwa. Katika kijiji hicho, watalii wanaweza kujionea uzalishaji wa kilimo, maisha ya wakulima na utamaduni wa kikabila."


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako