• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maisha mapya ya wafugaji wa Wakazakh katika sehemu ya Artai

    (GMT+08:00) 2009-11-19 16:45:17

    Katika mkoa unaojiendesha wa Xinjiang Uyghur, kuna makabila mbali mbali ya wafugaji wanaohamahama yakiwemo makabila ya Wakazakh, Wamongolia, Wakirghiz na Watajiki. Tokea zama za kale, wafugaji wa makabila hayo wamekuwa wakihamahama, ili kutafuta malisho na maji kwa ajili ya mifugo yao. Lakini maisha ya kuhamahama yanawafanya watu hao wakose huduma nzuri za matibabu na elimu. Hivi sasa serikali ya China imeanza kutekeleza mradi wa kuwajengea wafugaji wanaohamahama makazi ya kudumu.

    Katika tarafa ya Xiyganjiyde ya wilaya ya Fuhai iliyoko katika sehemu ya Artai, kuna familia zaidi ya 600 za wafugaji wa kabila la Wakazakh. Katika miaka elfu kadhaa iliyopita, wafugaji hao walikuwa wakiishi kwa kuhamahama. Bw. Regbai Chamar mwenye umri wa miaka 37 ni mkazi wa tarafa hiyo. Alisema zamani kila theluji inapoyeyuka, yeye na familia yake walihamisha mifugo katika mashamba ya mifugo ya majira ya mchipuko na mapukutiko kutoka mashamba ya mifugo ya majiar ya baridi, kuanzia mwezi Juni, walihamia mashamba ya majira ya joto, wakati theluji inapoanguka mwishoni mwa Agosti waliondoka milimani, na mwishoni mwa mwezi Novemba, walirudi kwenye mashamba ya majira ya baridi. Bw. Regbai alisema,

    "Zamani tulipokuwa tukifuga mifugo, tulihamahama mara kwa mara. Tulipokuwa wagonjwa, hatukuweza kupata matibabu kwa wakati, na hata watu wengi walifariki njiani."

    Njia hiyo ya jadi ya ufugaji si kama tu inawafanya wafugaji wakose huduma za afya na elimu, bali pia ilizidisha kuvia kwa mashamba ya mifugo, na kusababisha tatizo kubwa kwa shughuli za ufugaji. Ofisa mwandamizi wa sehemu ya Artai Bw. Zhang Handong alisema,

    "Zamani wafugaji walihama kwa zaidi ya mara 90 kila mwaka. Katika hali hiyo, je, wao wanayoelimika vipi? Na wanapata vipi huduma za afya? Hali hii iliwafanya wafugaji hao washindwe kunufaika na maendeleo ya jamii. Aidha ongezeko la watu na mifugo lilisababisha shinikizo kubwa kwa mazingira."

    Ili kuwasaidia wafugaji wanaohamahama kuondoa matatizo hayo, miaka kadhaa iliyopita, serikali ya China ilianza kuwapa ruzuku au makazi ya kudumu. Kijiji cha Saikelu kilichopo katika tarafa ya Xiyganjiyde ni sehemu ya makazi ya kudumu iliyojengwa na serikali kwa ajili ya wafugaji wa Wakazakh. Mwaka 2008, Bw. Regbai pamoja na wafugaji wengine wengi walihamia kijiji hicho. Waandishi wetu wa habari walipoingia nyumbani kwake, waliona vifaa mbalimbali vya vya kisasa kwenye chumba cha kuwapokea wageni zikiwemo televisheni, sofa, na pepeo ya umeme, na ukuta ukiwa umepambwa vizuri kwa vitambaa vyenye rangi nzuri.


    1 2
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako