Hivi sasa familia ya Bw. Regbai ina mashamba ya alizeti karibu hekta 7, na mifugo 150 wekiwemo ng'ombe 30 na mbuzi 120. Mbali na hayo Bw. Regbai anaendesha duka moja. Mwaka jana mapato ya familia yake yalifikia yuan elfu 36.
Katika tarafa ya Xiyganjiyde, kuna familia zaidi ya 300 za watu waliokuwa wafugaji wa kuhamahama. Ofisi mwandamizi wa tarafa hiyo Bw. Zhang Jianjiang alisema, kuwasaidia wafugaji hao kuisha maisha bila ya kuhamahama si kama tu kuwajengea makazi ya kudumu, alisema,
"Jambo muhimu la kwanza ni kukidhi mahitaji yao ya kulisha mifugo, ama sivyo watahama tena."
Bw. Zhang alijulisha kuwa, wafugaji wa tarafa ya Xiyganjiyde walianza kuweka makazi ya kudumu katika miaka ya 90 ya karne iliyopita, lakini wakati huo, mapato ya wafugaji hao yalikuwa kidogo, pia hawakuweza kupata huduma nzuri. Baada ya mwaka 2006, serikali iliongeza nguvu ya kuwasaidia, na kutoa yuan elfu 25 kwa kila familia ili kuwasaidia kujenga nyumba. Halafu ilijenga barabara nzuri na vyoo safi, na kuwapatia wakazi umeme, maji, radio na televisheni. Licha ya ufugaji wa kawaida, wakazi wa tarafa ya Xiyganjiyde pia wanaweza kujishughulisha na shughuli za upandaji na ufugaji wa wanyama maalumu.
Kuishi maisha bila ya kuhamahama si kama tu kumebadilisha mtindo wa uzalishaji na maisha ya wafugaji wa Wakazakh tu, bali pia kumewatolea mazingira mazuri ya kuishi, kufanya kazi na kuelimika. Zamani hakuwa na hospitali katika sehemu za milimani, wafugaji walioishi katika sehemu hizo wakiwa na ugonjwa, ni lazima waende kwenye hospitali iliyoko wilayani kwa kutembea kwa siku nzima na usiku mzima. Lakini hivi sasa hali imebabilika, watu hao wanaweza kupata huduma za afya kwenye vijiji wanavyoishi. Mbali na hayo, huduma ya elimu pia imeboreshwa sana. Watoto wa wafugaji wanaweza kusoma katika shule ya tarafa. Bw. Regbai alisema,
"Sikupata elimu, hata sijui lugha ya Putonghua, hivyo nimeshindwa kuwasiliana vizuri na watu kutoka sehemu za nje. Baada ya kuhamia hapa, mtoto wangu anaweza kusoma shuleni. Sasa yeye ni mwanafunzi wa mwaka wa nne katika shule ya msingi."
Katika sehemu ya Artai, kuna wafugaji karibu laki 1.5 wa kabila la Wakazakh, na hadi sasa theluthi moja kati yao wamehamia katika makazi ya kudumu. Kuwasaidia wafugaji kuishi maisha bila ya kuhamahama kunachukuliwa na serikali ya sehemu hiyo kuwa ni mradi muhimu zaidi. Ofisa mwandamizi wa sehemu hiyo Bw. Zhang Handong alisema, serikali itaendelea na juhudi ili kuwafanya wafugaji waishi maisha bora zaidi, alisema,
"Vitu viwili muhimu katika kuwahamasisha wafugaji waache kuhamahama ni mitaji na ardhi. Mwaka huu serikali kuu imetenga yuan milioni 32 kwa tarafa yetu, na kila familia ya wafugaji ilipata ruzuku ya yuan elfu 25. Hatua ijayo tutatoa ardhi kwa familia hizo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |