• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Utengenezaji na uuzaji wa magari nchini China watazamiwa kuendelea kuongezeka kwa kasi mwaka huu

    (GMT+08:00) 2010-01-27 10:06:24

    Mwaka 2009 utengenezaji na uuzaji wa magari ulizidi milioni 13.5 nchini China, ambao ulichukua nafasi ya kwanza duniani kwa mara ya kwanza badala ya Marekani. Lengo hili limetimizwa miaka mitano hadi sita mapema kuliko ilivyokadiriwa. Wahusika wanasema mwaka huu utengenezaji na uuzaji wa magari nchini China utaendelea kuongezeka kwa kasi, na unatazamiwa kuzidi magari milioni 15.

    Mwaka jana shughuli za utengenezaji wa magari zilikuwa moja kati ya shughuli muhimu zinazohimiza ongezeko la uchumi wa China. Utengenezaji wa magari ulifikia magari milioni 13.8, na uuzaji wa magari ulifikia magari milioni 13.65, wote ukiwa na ongezeko la asilimia 50 hivi kuliko mwaka juzi. Kutokana na utekelezaji wa sera ya kupunguza nusu ya kodi kwa magari yenye ujazo wa ijini usiozidi lita 1.6, uuzaji wa magari ya aina hiyo ulifikia milioni 7.2, ambao uliongezeka kwa zaidi ya asilimia 70. Mchambuzi wa shughuli za magari za China Bw. Jia Xinguang alifahamisha kuwa mwelekeo mzuri wa uchumi wa jumla na utekelezaji wa sera za kuchochea ununuzi wa magari umehimiza ongezeko kubwa la uuzaji wa magari nchini China, akisema,

    "Mwaka jana uchumi wa jumla wa China uliongezeka kwa zaidi ya asilimia 8, ambao ulisukuma mbele ongezeko la uuzaji wa magari. Serikali kuu ilitunga sera tatu za kuhimiza uuzaji wa magari, zikiwemo sera za kupunguza nusu ya kodi ya kununua magari, kuwasaidia wakulima kununua magari, pesa kidogo kununua magari mapya kwa yale makukuu."

    Ingawa sera hizo zimetoa mchango mkubwa kwa ongezeko kubwa la uuzaji wa magari nchini China, lakini baadhi ya watu wanaona kuwa ongezeko kubwa kupita kiasi la uuzaji wa magari litapunguza mauzo ya magari kwa mwaka huu.

    Kampuni ya utafiti na utoaji ushauri ya Lingdian ilifanya uchunguzi kuhusu suala hili, na inaona kuwa mahitaji ya magari yataufanya uuzaji wa magari uendelee kuongezeka kwa kasi katika muda mrefu ujao. Meneja mkuu wa kampuni hiyo Bw. Yuan Yue alisema wastani wa pato la taifa kwa kila mtu umezidi dola za kimarekani 3000. Kwa kawaida hali hii inamaanisha kuwa China itaingia kwenye kipindi chenye ununuzi mkubwa wa magari. Familia nyingi za China zitanunua magari, hivyo ongezeko la uuzaji wa magari litaendelea. Bw. Yuan alisema,

    "Familia nyingi za China zitaanza kununua magari, na hali hii huenda itaendelea kwa miaka 50 hadi 60. Hali nchini China ni tofauti na hali ya nchi za magharibi ambazo kiwango cha maendeleo ya viwanda ni cha juu."

    Mwaka jana, licha ya suala la msukosuko wa fedha duniani, suala la mabadiliko ya hali ya hewa pia lilikuwa moja kati ya masuala yanayofuatiliwa na watu wengi. Mkutano wa Copenhagen uliojadili njia ya kupunguza utoaji wa hewa zinazosababisha kuongezeka kwa joto duniani, ulionesha watu wengi duniani wanafuatilia kubana matumizi ya nishati. Katika hali hiyo, usanifu na utengenezaji wa magari yanayotumia nishati mpya umekuwa kazi muhimu ya makampuni ya magari duniani. Naibu meneja mkuu wa kampuni ya Geely ya mkoa wa Zhejiang Bw. Zhao Fuquan alifahamisha kuwa, mwaka huu kampuni hiyo itaonesha teknolojia za kizazi cha tatu za magari yanayotumia nishati mpya, akisema,

    "Usanifu wa magari yanayotengenezwa kwa teknolojia za kizazi cha kwanza na cha pili umemalizika, hivi sasa tunashughulikia utengenezaji wa magari kwa kutumia teknolojia za kizazi cha tatu, yaani kutengeneza magari yanayotumia umeme na nishati ya jua. Mwaka huu tutaonesha bidhaa hizo kwenye maonesho ya magari ya Beijing."


    1 2
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako